Wafanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete wapongezwa kwa utendaji mzuri wa kazi

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Utawala na Fedha wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA Agnes Kuhenga akisoma majina ya wafanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 wa Taasisi hiyo ambapo wafanyakazi watatu walichaguliwa na kupewa zawadi mbalimbali za kuwapongeza kutokana na  utendaji wao mzuri wa kazi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi zawadi ya ngao mfanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 aliyeshika nafasi ya kwanza George Msabila wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora watatu iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Mfanyakazi huyo pia alipewa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni moja na laki tano.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi zawadi ya cheti  mfanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 aliyeshika nafasi ya pili Dkt. Henry Mayala wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora watatu iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Mfanyakazi huyo pia alipewa zawadi ya fedha taslimu shilingi laki nane.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi zawadi ya cheti  mfanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 aliyeshika nafasi ya tatu  Danford Mrope wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora watatu iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Mfanyakazi huyo pia alipewa zawadi ya fedha taslimu shilingi laki tano.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 wa Taasisi hiyo mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuwapongeza iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi mfanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 aliyeshika nafasi ya kwanza  George Msabila zawadi iliyotoka kwa kampuni ya uingizaji na usambazaji wa dawa za binadamu ya  Samiro Pharmaceutical Ltd. Kampuni ya Samiro huwa inatoa zawadi kwa wafanyakazi bora wa Taasisi hiyo ikiwa ni njia moja wapo ya kuwapa motisha ya kazi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi mfanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 aliyeshika nafasi ya pili Dkt. Henry Mayala zawadi  iliyotoka kwa kampuni ya uingizaji na usambazaji  dawa za binadamu ya  Samiro Pharmaceutical Ltd. Kampuni ya Samiro huwa inatoa zawadi kwa wafanyakazi bora wa Taasisi hiyo  ikiwa ni njia moja wapo ya kuwapa motisha ya kazi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi mfanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 aliyeshika nafasi ya tatu  Danford Mrope zawadi  iliyotoka kwa kampuni ya uingizaji na usambazaji wa dawa za binadamu ya  Samiro Pharmaceutical Ltd. Kampuni ya Samiro huwa inatoa zawadi kwa wafanyakazi bora wa Taasisi hiyo  ikiwa ni njia moja wapo ya kuwapa motisha ya kazi.

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Utawala na Fedha wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA Agnes Kuhenga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kurugenzi hiyo mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora wa  robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21.  Wa pili kushoto ni mfanyakazi aliyeshika nafasi ya tatu  mhasibu Danford Mrope aliyotoka katika kurugenzi ya Utawala na Fedha.

Baadhi ya wafanyakazi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia tukio la utoaji wa zawadi kwa  wafanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 wa Taasisi hiyo ambapo wafanyakazi watatu walichaguliwa na kupewa zawadi mbalimbali za kuwapongeza kutokana na  utendaji wao mzuri wa kazi.

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari