Serikali yawashukuru wataalamu wa afya nchini kwa kutoa huduma bora za matibabu kwa wagonjwa - Dkt. Mollel
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Godwin Mollel akizungumza na wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara yake ya kikazi katika Taasisi hiyo Jana Jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Godwin Mollel akizungumza na madaktari wa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) waliokuwa wakiwaudumia wagonjwa waliolazwa wodini wakati wa ziara yake ya kikazi katika Taasisi hiyo Jana Jijini Dar es Salaam. Na: JKCI Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel amewashukuru wataalamu wa afya nchini kwa moyo wao wa uzalendo wa kutoa huduma bora za matibabu kwa wagonjwa. Mhe. Mollel ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaja Kikwete (JKCI) aliowakuta wanawatibu wagonjwa wodini na kliniki wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya leo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam....