Wafanyakazi bora wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2020/21 wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete wapongezwa kwa utendaji mzuri wa kazi

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi zawadi ya ngao mfanyakazi bora wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2020/2021 aliyeshika nafasi ya kwanza Mtoka David Mtoka wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora watatu iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Mfanyakazi huyo pia alipewa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni mbili



Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti mfanyakazi bora wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2020/2021 aliyeshika nafasi ya pili Mohamed Songoro wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora watatu iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Mfanyakazi huyo pia alipewa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni moja na laki tano


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti mfanyakazi bora wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2020/2021 aliyeshika nafasi ya tatu Lucas Jilulu wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora watatu iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Mfanyakazi huyo pia alipewa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni moja.


Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Utawala na Fedha wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA Agnes Kuhenga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Kurugenzi hiyo pamoja na wafanyakazi wa kitengo cha Ununuzi na Ugavi mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora wa robo ya pili ya mwaka wa fedha wa 2020/2021. Wapili kushoto ni mfanyakazi aliyeshika nafasi ya kwanza Mtoka David Mtoka aliyetoka katika kurugenzi ya Utawala na Fedha, wapili kulia ni mfanyakazi aliyeshika nafasi ya pili Mohamed Songoro aliyetoka katika kurugenzi ya Utawala na Fedha na katikati ni mfanyakazi aliyeshika nafasi ya tatu Lucas Jilulu aliyetoka katika kitengo cha Ununuzi na Ugavi.


 

Comments

Popular posts from this blog

Wateja wa CRDB kutibiwa JKCI kwa punguzo la asilimia 50%

Wanawake wa JKCI SACCOS wanaongoza kwa kumiliki hisa

JKCI, MOI NA MNH waitwa Comoro kutoa huduma za matibabu ya kibingwa