Ukuaji wa teknolojia wachochea ufanisi matibabu ya moyo

Baadhi ya wadau wa sekta ya afya wakifuatilia mada inayohusu magonjwa ya moyo wakati wa mdahalo wa kitaaluma (Symposium) uliofanyika jana katika kituo cha mikutano cha Jakaya Kikwete katika kuadhimisha ya wiki ya Afya kitaifa **************************************************************************************** Imeelezwa kuwa ukuaji na maendeleo ya Teknolojia umechochea kwa kiwango kikubwa katika ufanisi wa kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo hapa nchini. Hayo yamebainishwa jana Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Upasuaji wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya wakati akitoa wasilisho kwenye mdahalo wa Kitaaluma (Symposium) uliofanyika wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Afya Kitaifa. Dkt. Angela alisema matumizi ya Teknolojia yamekuwa na ufanisi mkubwa kwenye matibabu ya magonjwa ya moyo kwani kwa kutumia simu Janja App mwananchi anaweza kupima mapigo ya moyo, shinikizo la damu na umeme wa moyo. “Serika...