JKCI yawafanyia uchunguzi wa afya wafanyakazi 134 wa Bohari ya Dawa (MSD)
Daktari kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Edward Martin akizungumza na mfanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD) Doreen Josiah mara baada ya kufanya uchunguzi wa afya wakati wa kambi maalumu ya siku ya mbili iliyokuwa ikifanywa na wataalamu kutoka JKCI na kumalizika jana katika Ofisi za MSD zilizopo jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa Maabara kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Daniel Munishi akimpima wingi wa sukari katika damu mfanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD) Ziada Athumani wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya uchunguzuzi wa afya iliyokuwa ikifanywa na wataalamu kutoka JKCI na kumalizika jana katika Ofisi za MSD zilizopo jijini Dar es Salaam.
Picha
na: Khamis Mussa
********************************************************************************************************************
Wafanyakazi 134 wa Bohari ya Dawa (MSD) wamefanyiwa uchunguzi wa magonywa ya moyo, homa ya ini na Virusi vya ukimwi (VVU) na wataalamu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Uchunguzi huo umefanyika wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba iliyomalizika jana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali katika kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wafanyakazi wa MSD
wameishukuru Serikali kupitia Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kuona
umuhimu wa kufikisha huduma hizo mahali pa kazi na kutoa motisha kwa
wafanyakazi kuchunguza afya zao.
Mfamasia wa MSD Peace
Nyakojo alisema hatua ya kuwafuata wafanyakazi mahali pa kazi na kuwafanyia
uchunguzi wa afya umewasaidia kwa kiasi kikubwa kufahamu hali zao za afya na
kuchukua hatua za kujilinda dhidi ya magonja yasiyoambukiza.
“Naishukuru sana JKCI kwa
kutufikishia huduma hizi, tumeelimishwa kuhusu hatari zinazoweza kuwapata
wafanyakazi wa mijini na mambo mengine mengi, ninawaomba zoezi hili lisiishe
hapa kwetu bali liweze kuwafikia wafanyakazi wenzetu waliopo katika kanda zote”,
alisema Peace
“Nimefurahia huduma hii kwani tumezoea kupanga
foleni hospitalini ili kupata huduma lakini leo bila foleni tumepata huduma kwa
wakati, hata upande wa chanjo ya home ya ini hatukuwa tunaichukulia kwa umuhimu
hadi baada ya kupata elimu ndio tumeona ni muhimu kupata chanjo hii”, alisema Norah Osei-Kumi, Mwanasheria wa
Bohari ya Dawa (MSD)
“Tangu nimezaliwa sijawahi kupima afya ya
moyo, changamoto za afya na vifo vya ghafla vimekuwa vingi hivyo inopotokea
huduma kama hizi tusidharau tujitokeze kwa wingi kuchunguza afya zetu”, alisema
Winifrida Milanzi, Afisa Ugavi wa
Bohari ya Dawa (MSD).



Comments
Post a Comment