Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Aloycia Lyimo akimpima kiwango cha sukari mwilini mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo jana katika viwanja vya MwembeYanga wilayani Temeke kupitia jukwaa la One Stop Jawabu ambapo JKCI ilitoa bila malipo huduma za upimaji, matibabu na ushauri wa magonjwa ya moyo kwa watu 150. Septemba 24, 2020 – DAR ES SALAAM Jumla ya watu 150 wamejitokeza na kufanyiwa uchunguzi na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), watu 37 kati ya hao wamekutwa na shinikizo la damu, 19 walikuwa hawajijui hali zao hapo kabla. Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa JKCI, Samweli Rweyemamu alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari alipokuwa akieleeza tathmini kuhusu huduma ya uchunguzi na tiba waliyoitoa kwa wakazi wa Temeke, Septemba 18 na 23, mwaka huu, Viwanja vya Mwembe Yanga na Zakheem, kwenye Jukwaa la One Stop Jawabu. “Mwamko na mwitiko wa wananchi umekuwa mkubwa, juzi kule Zakheem tuliona watu 103, ...