Waumini wa Jumba la Ufalme wa Mashahidi wa Yehova waishukuru JKCI kwa kumfanyia upasuaji mkubwa wa moyo na kumbadilisha ‘aortic valve’ ambayo inatoa damu kutoka kwenye moyo kwenda mwilini na kumuwekea valvu nyingine ya chuma muumini wa dhehebu hilo bila ya kumuongezea damu


Mwanakamati wa Halmashauri ya Mahusiano na Hospitali wa Jumba la Ufalme wa Mashahidi wa Yehova, Godliving Makundi akizungumza wakati wa mkutano baina yao na uongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Wanakamati hao walitembelea JKCI kwa ajili ya kuwashukuru kwa kumfanyia muumini wa dhehebu hilo upasuaji mkubwa wa moyo wa kubadilisha valvu bila ya kumuongezea damu. Kulia ni Mkurugenzi wa JKCI Prof. Mohamed Janabi.

Baadhi ya viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Wanakamati wa Halmashauri ya Mahusiano na Hospitali wa Jumba la Ufalme wa Mashahidi wa Yehova wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi akizungumza jinsi Taasisi hiyo inavyoheshimu imani za dini mbalimbali wakati wa mkutano baina yao uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza jambo na Mwanakamati wa Halmashauri ya Mahusiano na Hospitali wa Jumba la Ufalme wa Mashahidi wa Yehova Mashaka Mfala. Wanakamati hao walitembelea  JKCI kwa ajili ya kuwashukuru kwa  kumfanyia upasuaji mkubwa wa moyo na kubadilisha valvu muumini wa dhehebu hilo bila ya kumuongezea damu.

Waumini wa Jumba la Ufalme wa Mashahidi wa Yehova wameuomba uongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), kuendelea kuwapokea na kuwatibu wagonjwa wao pamoja na kuwapa ushauri wa kimatibabu. 

Dhehebu hilo limeipa pongezi za dhati uongozi wa JKCI na wafanyakazi wake kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya kwa kumtibu muumini wao, Ayubu Ngonyani (24), tatizo la moyo lililokuwa likimsumbua kwa kumfanyia upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo bila kumuongezea damu. 

Muumini huyo alipokewa JKCI Juni, mwaka huu akiwa hawezi kutembea umbali mrefu bila kupumzika, alihisi mwili wake kuchoka, alihisi kukosa pumzi na alikuwa hawezi kulala vema pasipo kutumia mito mitatu au minne. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo hospitalini hapo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji waJKCI,Prof. Mohamed Janabi alisema uchunguzi ulibaini kwamba ‘valve’ moja ya moyo ilikuwa imeharibika mno. 

“Hakukuwa na namna nyingine yoyote kumtibu isipokuwa kufanyiwa upasuaji mkubwa kuibadilisha, moyo una ‘valve’ nne, sasa ile ‘aortic valve’ ambayo yenyewe ni kubwa inayotoa damu kutoka kwenye moyo kwenda mwilini ndiyo ilikuwa imeharibika kabisa, haikuwezekana ‘ku – repair’, ililazimu kuiondoa na kumuwekea ‘valve’ mbadala ‘ya chuma’. 

“Lakini tulipomueleza kile tulichobaini baada ya uchunguzi wa vipimo, Ayubu alisema yeye ni muumini wa imani ya Mashahidi wa Yehova na kwa mujibu wa imani yake, huwa hawaongezewi damu, ilitupa changamoto,” alisema. Prof. Janabi 

Alisema waliridhia ombi la mgonjwa huyo na kuandaa utaratibu wa matibabu yake. “Kwa kumuomba Mwenyezi Mungu na kwa kutumia mitambo ya kisasa iliyosimikwa ndani ya taasisi hii, Wataalamu wetu mabingwa waliweza kumfanyia upasuaji bila kusimamisha moyo (ukiwa unadunda vile vile) na bila kumuongezea damu, waliweza kufanikisha upasuaji wake kwa ufanisi mkubwa,” alisema. 

“Moyo una ‘valve’ nne, sasa ile ‘aortic valve’ amb ayo yenyewe ni kubwa inayotoa damu kutoka kwenye moyo kwenda mwilini, ilikuwa imeharibika kabisa, haikuwezekana ‘ku – repair’, ililazimu kuiondoa na kumuwekea ‘valve’ mbadala ‘ya chuma’. 

“Kwa kumuomba Mwenyezi Mungu na kwa kutumia mitambo ya kisasa iliyosimikwa ndani ya taasisi hii, Wataalamu wetu mabingwa waliweza kumfanyia upasuaji bila kusimamisha moyo (ukiwa unadunda vile vile) na bila kumuongezea damu, waliweza kufanikisha upasuaji wake kwa ufanisi mkubwa,” amesema. 

Mwanakamati wa Halmashauri ya Mahusiano na Hospitali wa Jumba la Ufalme wa Mashahidi wa Yehova, Godliving Makundi alisema mafanikio hayo yamewapa tumaini kwamba sekta ya afya Tanzania, imeimarika na huduma hiyo inawezekana kupatikana nchini. 

“Ayubu hali yake ni njema, hii sisi imetugusa moyo sana na ndilo limetusukuma kuja hapa JKCI leo kutoa shukrani zetu za dhati kwa uongozi na wafanyakazi kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya kwa mgonjwa wetu. 

“Tunawashukuru kwa moyo wao wa k itabibu na kutuelewa kutumia taaluma yao kwa kadri wanavyoweza ili kuendelea kusaidia wagonjwa wetu waendelee kuishi na kufurahia maisha kama wagonjwa wengine huku imani yao na dhamiri yao ikiwa imebaki safi,” alisema. 

Aliuomba uongozi wa JKCI kuendelea kupokea wagonjwa wao na kuwapa matibabu kwa kadri itakavyoonekana kuwafaa. 

“Kwa vile wao tayari wamepata uzoefu, tutakuwa tunawaelekeza wagonjwa wetu wenye matatizo ya moyo kuja kupata ushauri na tiba hapa Taasisi ya Moyo,” alisema. 

Kuhusu ombi la Kamati hiyo, Prof. Janabi alisema wamelikubali na wapo tayari kuendelea kuwapokea waumini hao na kuwatibu kama ambavyo huwa wanapokea na kuwatibu waumini wa imani nyingine mbalimbali kwani Taasisi hiyo inaheshimu imani za dini za watu. 

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari