Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) yawaibua watu 21 wenye shida mbalimbali za moyo, 18 wakutwa na Shinikizo la Damu, zaidi ya asilimia 50 wana uzito uliopitiliza, Jukwaa la One Stop Jawabu - MBAGALA
Daktari wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Samwel Rweyemamu akimpatia dawa mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo kwa ajili
ya kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo
na kukutwa na tatizo. Uchunguzi huo ulifanyika hivi karibuni katika
viwanja vya Mbagala Zakheem wilayani Temeke kupitia jukwaa la One Stop Jawabu ambapo wananchi 103 walifika katika banda hilo
na kupewa huduma za ushauri na upimaji wa magonjwa ya moyo.
DAR ES SALAAM
TAASISI ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), imewaibua watu 21 wenye matatizo mbalimbali ya moyo, 18 wamekutwa na shinikizo la damu, walipochunguzwa afya zao katika Viwanja vya Mbagala Zakheem wilayani Temeke kwenye jukwaa la One Stop Jawabu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Daktari Bingwa wa Magonjwa
ya Moyo wa JKCI, Samweli Rweyemamu alisema watu 16 kati ya 18 waliokutwa
na shinikizo la damu walikuwa hawajitambui kwamba wanakabiliwa na tatizo hilo.
“Hii ni sawa na asilimia 18, yupo mmoja ambaye tumemkuta ana
shinikizo la damu 200 chini ya 110, ni mara yake ya kwanza amekuja kufanyiwa
uchunguzi, ni shinikizo ambalo lipo juu mno, tulidhani labda amepata mshtuko
alipofika hapa.
“Tulimtaka akae kidogo apumzike, tukamfanyia tena uchunguzi na
kukuta hali ikiwa vile vile, endapo tusingemgundua alikuwa kwenye hatari kubwa
ya kupoteza maisha, tumempa rufaa kuja JKCI kwa matibabu,” amebainisha.
Dk. Rweyemamu amesema mtu mmoja kati ya hao walifanyiwa
uchunguzi amekutwa na tatizo la kuziba kwa mshipa wa damu kwenye moyo, watu 10
wamekutwa na kisukari.
“Watu 50 tuliwachunguza afya ya moyo kwa kutumia kipimo cha kuangalia
jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography - ECHO) na 53 tuliwafanyia kipimo
cha kuangalia umeme wa moyo (Electrocardiography - ECG) wawili kati ya hao tuliowachunguza tulikuta
‘valve’ zao za moyo zina tatizo,” amebainisha.
Ameongeza “Asilimia 50 ya watu wote tuliowachunguza wana uzito
uliopitiliza, hii ni hatari kwa afya ya mioyo yao. Watu 21 tumewapa rufaa kuja
kwenye Taasisi yetu kupitia Hospitali yao ya Mbagala Zakheem ili tuwafanyie
uchunguzi zaidi na kuwapa matibabu.
Amesema ndani ya banda lao pamoja na uchunguzi wa afya ya moyo,
vile vile walitoa elimu ya lishe kwa wananchi hao ili waweze kulinda afya yao
ya moyo na mwili kwa ujumla.
“Tumewaelimisha wazingatie ulaji unaofaa, waepuke vyakula vyenye
mafuta mengi, chumvi nyingi, sukari nyingi na uvutaji wa sigara, ili kuepuka
magonjwa yasiyo ambukiza ikiwamo haya ya moyo.
“Tumewashauri pia kukata bima ya afya ili wawe na uhakika wa
kupata matibabu maana gharama ni kubwa endapo ukiwa huna bima ya afya ni
changamoto,” amesema.
Wakizungumza mara baada ya kupatiwa huduma katika banda la
Taasisi hiyo wakazi wa Mbagala ameipongeza Serikali na Ofisi ya Mkuu wa
Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe kwa kupeleka jukwaa hilo katika eneo hilo kwani
wameweza kufikiwa na kufanyiwa uchunguzi wa afya ya moyo na hatimaye wengine
wamelutwa na matatizo na kupewa huduma ya matibabu.
“Kupitia vyombo vya habari nilisikia siku ya leo wataalamu wa
moyo watakuwepo mahali hapa nikaamua kuja kupima afya yangu. Nimeweza kupima na
kufahamu hali yangu ikoje. Ninashukuru sana kwa huduma niliyoipata”,.
“Ninawashauri wananchi wenzangu wanaposikia wataalamu kama hawa wanafanya upimaji wajitokeze kwa wingi kupima afya zao kwani kwa kufanya hivyo kutawasaidia kufahamu wanakabiliwa na matatizo gani ili waweze kupata matibabu kwa wakati na kama hawana matatizo wataweza kujikinga”, alisema Hamza Juma mkazi wa Chamazi.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Zenais Ngowi akitoa maelekezo ya jinsi ya kujaza fomu ya uelewa wa magonjwa ya moyo kwa mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo katika viwanja vya Mbagala Zakheem wilayani Temeke kupitia jukwaa la One Stop Jawabu ambapo Taasisi hiyo ilitoa bila malipo huduma za upimaji, matibabu na ushauri wa magonjwa ya moyo.Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Steven Lugu akimpima shinikizo la damu (BP) mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo katika viwanja vya Mbagala Zakheem wilayani Temeke kupitia jukwaa la One Stop Jawabu ambapo wananchi 103 walifika katika banda hilo na kupewa huduma za ushauri na upimaji wa magonjwa ya moyo.Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Zenais Ngowi akitoa maelekezo ya jinsi ya kujaza fomu ya uelewa wa magonjwa ya moyo kwa mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo katika viwanja vya Mbagala Zakheem wilayani Temeke kupitia jukwaa la One Stop Jawabu ambapo Taasisi hiyo ilitoa bila malipo huduma za upimaji, matibabu na ushauri wa magonjwa ya moyo.
Wananchi waliofika katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika viwanja vya Mbagala Zakheem wilayani Temeke kupitia jukwaa la One Stop Jawabu wakipata huduma mbalimbali za upimaji, matibabu na ushauri wa magonjwa ya moyo ambapo watu 103 walifika katika banda hilo na kupewa bila malipo huduma za ushauri na upimaji wa magonjwa ya moyo.Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji akimpa mwananchi elimu ya lishe bora kwa afya ya moyo wakati wa jukwaa la One Stop Jawabu lililofanyika katika viwanja vya Mbagala Zakheem wilayani Temeke kupitia Jukwaa la One Stop Jawabu ambapo Taasisi hiyo ilitoa bila malipo huduma za upimaji, matibabu na ushauri wa magonjwa ya moyo.
Comments
Post a Comment