TUGHE- JKCI yaishukuru menejimenti ya JKCI kwa uongozi sikivu

Mhadhiri wa chuo kikuu cha Tumaini Dkt. Mtaki akitoa mada ya sheria za kazi kwa wajumbe wa kikao cha nne cha baraza la wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. Baraza huru na uongozi sikivu wa menejimenti ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inayoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Profesa Mohamed Janabi ni mafanikio makubwa ambayo uongozi wa Baraza la nne la Wafanyakazi wa Taasisi hiyo umejivunia hatua ambayo imetajwa kuimarisha utendaji kazi na kuboresha huduma kwa wananchi. Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo wakati wa kikao cha nne cha baraza baraza la wafayakazi kilichofanyika Protea Hotel jijini hapa, Katibu wa chama cha wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya (TUGHE) tawi la JKCI, Joyce Mugala amesema Menejimenti hiyo imekuwa ikipokea hoja zao na kuzifanyia kazi kwa wakati. “Limekuwa baraza lenye mafanikio, tumeona Mkurugenzi Mtendaji amekuwa akipokea na kufan...