Madaktari Bingwa watatu wa China waagwa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) baada ya kumaliza muda wao wa kufanya kazi nchini
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi pamoja na wafanyakazi wa taasisi hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na madaktari bingwa wa moyo kutoka nchini China mara baada kumaliza kuwaaga kutokana na muda wao wa kufanya kazi kwa zaidi ya miaka miwili katika Taasisi hiyo kumaliza. Mwezi wa sita mwaka 2018 Serikali ya China ilitoa madaktari bingwa kuja kufanya kazi hapa nchini wakiwemo madaktari bingwa watatu wa magonjwa ya moyo.
Na Mwandishi Maalum – Dar es SaamOktoba
16, 2020 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), imewaaga madaktari bingwa
watatu wa magonjwa ya moyo ambao walitolewa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa
China kuja Tanzania kutoa huduma za matibabu ya moyo.
Serikali
ya Jamhuri ya Watu wa China kila baada ya miaka miwili huwa inatoa wataalamu
wake kwenda nchi mbalimbali Barani Afrika kutoa huduma za matibabu.
Madaktari
hao akiwamo daktari bingwa wa wagonjwa
walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU), daktari bingwa wa magojwa ya
moyo kwa watoto na daktari bingwa wa
upasuaji wa moyo walikuwapo
nchini baada ya kusainiana makubaliano hayo kati ya Serikali yao na Tanzania
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Akizungumza
wakati wa hafla ya kuwaaga madaktari hao mapema hii leo, Mkurugenzi Mtendaji wa
JKCI, Profesa Mohamed Janabi, amesema madaktari hao wamemaliza muda wa kufanya
kazi nchini.
“Walikuwapo
kwa kipindi cha miaka miwili tangu tarehe 22 Juni, 2018 hadi kufikia mwaka huu.
“Wanatarajia
kurudi nchini kwao katikati ya mwezi Oktoba, mwaka huu,tumejifunza mengi kutoka
kwao, tumeshirikiana nao kwa ukaribu, niliwaona ni sehemu ya timu yetu ya
wataalamu mabingwa wa JKCI,” amesema.
Ameongeza
“Wanarudi nchini kwao, tutaendelea kuwakumbuka kwa kazi nzuri waliyofanya
pamoja nasi, hakika walishirikiana nasi kwa ukaribu , wameshakamilisha taratibu
za kusafiri kurudi China.
“Wanapoondoka
tunatarajia timu nyingine ya wataalamu kutoka China ambao wameshakamilisha
taratibu za kuja nchini, tutaungana nao kuendelea kuimarisha huduma zetu,”
amebainisha.
Akizungumza
kiongozi wa timu hiyo ya madaktari kutoka China, waliokuja nchini kushirikiana na JKCI, Dk.
Qin Chengwei, amesema kipindi hicho ya mashirikiano kimekuwa chenye manufaa kwa
pande zote mbili.
“Binafsi
naona miaka miwili imeisha haraka mno, mmeshirikiana vizuri mno na wataalamu
wetu, tunashukuru, kwa zaidi ya miaka 50 sasa Serikali yetu imekuwa ikituma
madaktari nchi mbalimbali za Afrika.
“Tunaahidi
kuendelea kushirikiana na kuipa kipaumbele Tanzania, Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete, kuendelea kuleta wataalamu wetu kufanya nao kazi,” amesema.
Mmoja
wa madaktari hao ambaye ni daktari bingwa wa upasuaji wa moyo Hu Bin ameshukuru
uongozi wa Taasisi hiyo na wafanyakazi wote kwa kufanya nao kazi vizuri na kwa
ukaribu katika kipindi chote walichoishi nchini.
“Niliishi hapa kama nyumbani, mmekuwa nasi katika nyakati zote, kila hatua, hakika niliona JKCI ni hospitali yangu, ya maisha yangu,” amesema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi zawadi ya ngao yenye ramani ya Tanzania na cheti daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka nchini China Hu Bin ikiwa ni ishara ya kumshukuru baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi kwa zaidi ya miaka miwili katika taasisi hiyo. Kulia ni kiongozi wa madaktari hao ambaye pia ni Daktari bingwa wa usingizi Qin Chengwei anayefanya kazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi zawadi ya ngao yenye ramani ya Tanzania daktari bingwa wa magojwa ya moyo kwa watoto kutoka nchini China Zhao Lijian ikiwa ni ishara ya kumshukuru baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi kwa zaidi ya miaka miwili katika Taasisi hiyo. Katikati ni kiongozi wa madaktari hao ambaye pia ni Daktari bingwa wa usingizi Qin Chengwei anayefanya kazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi zawadi ya picha yenye mchoro wa tingatinga daktari bingwa wa wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini China Cui Jian ikiwa ni ishara ya kumshukuru baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi katika Taasisi hiyo. Mwezi wa sita mwaka 2018 Serikali ya China ilitoa madaktari bingwa 11 kuja kufanya kazi hapa nchini wakiwemo madaktari bingwa watatu wa magonjwa ya moyo.
Kiongozi wa madaktari kutoka nchini China ambao wanafanya kazi hapa nchini ambaye pia ni Daktari bingwa wa usingizi Qin Chengwei katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akiishukuru menejimenti ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa jinsi walivyoshirikiana na Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo watatu ambao wamefanya kazi katika Taasisi hiyo kwa zaidi ya miaka miwili.
Madaktari Bingwa wa magojwa ya moyo kutoka nchini China wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuagwa na Menejimenti ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambako walikuwa wanafanya kazi kwa zaidi ya miaka miwili. Mwezi wa sita mwaka 2018 Serikali ya China ilitoa madaktari bingwa 11 kuja kufanya kazi hapa nchini wakiwemo madaktari bingwa watatu wa magonjwa ya moyo.
Comments
Post a Comment