TUGHE- JKCI yaishukuru menejimenti ya JKCI kwa uongozi sikivu

Mhadhiri wa chuo kikuu cha Tumaini Dkt. Mtaki akitoa mada ya sheria za kazi  kwa wajumbe wa kikao cha nne cha  baraza la wafanyakazi wa   Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Baraza huru na uongozi sikivu wa menejimenti ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  inayoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Profesa Mohamed Janabi ni mafanikio makubwa ambayo uongozi wa Baraza la nne la Wafanyakazi wa Taasisi hiyo umejivunia hatua ambayo imetajwa kuimarisha utendaji kazi na kuboresha huduma kwa wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo wakati wa kikao cha nne cha  baraza  baraza la wafayakazi kilichofanyika Protea Hotel jijini hapa, Katibu wa chama cha wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya (TUGHE)  tawi la  JKCI, Joyce Mugala amesema Menejimenti hiyo imekuwa ikipokea hoja zao na kuzifanyia kazi kwa wakati.

“Limekuwa baraza lenye mafanikio, tumeona Mkurugenzi Mtendaji amekuwa akipokea na kufanya yale tunayojadili na kutupa mrejesho kwa wakati, limekuwa baraza sikivu kwani menejimenti imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na wafanyakazi hususan kwa upande wa maslahi,” amesema.

Joyce ameongeza “Kama mnavyojua mgogoro mkubwa wa wafanyakazi ni maslahi na uongozi, lakini tunashukuru Mkurugenzi Mtendaji wetu amekuwa msikivu anatupa kile tunachowasilisha kwa mfano posho kwa wafanyakazi tuliomba kwenye kikao alilichukua na tukapewa kwa wakati,” ametoa mfano.

Joyce ameongeza “Sisi wafanyakazi tunajivunia limekuwa Baraza 'productive' maana yale tunayoshauriana na uongozi yanatendewa kazi.

“Vitendea kazi JKCI is perfect hatuna tatizo lolote kwa upande huo, kuanzia mazingira ya ofisi, utendaji 'Theater' na 'Cathlab' watu wapo 'happy', kutokana na mazingira ya ofisi na vitendea kazi.

“Menejimenti imejali mpaka kufikia hatua ya kuongeza 'Cathlab' nyingine, tunashukuru pale tunapohitaji kitu, inasikia na kuyafanyia kazi, hii ni maabara ambayo mtaalamu anaweza kuuchunguza moyo ulivyo na kuweza kutibu inapohitajika.

“Furaha ya Watanzania ni pale JKCI inapotoa huduma bora na nzuri kwao, tunakwenda kutoa huduma Bora zaidi,” amesisitiza Joyce.

Naye, Ofisa Ugavi Msaidizi wa JCKI ambaye pia ni mjumbe wa baraza hilo, Rajabu Nasibu amesema kwa upande wa manunuzi kumekuwa na mafanikio Taasisi imepiga hatua kubwa kimaendeleo.

“Tulipoanza ilikuwa Taasisi changa mwendo wake ulikuwa ukisuasua, hatukuwa na vifaa kama tulivyonavyo sasa, tumepiga hatua, malengo yanaongezeka hata kwa upande wa manunuzi ya vifaa tiba awali watu binafsi ndiyo walikuwa wanavileta nchini sasa hivi Serikali ndiyo inayoagiza na kuleta moja kwa moja nchini,” amesema.

Akizungumza Prof. Janabi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo amesema limekuwa kiunganishi kikubwa kati ya wananchi, wafanyakazi na menejimenti ya Taasisi hiyo.

“Tunajivunia utulivu mkubwa uliopo kwenye Baraza hili, menejimenti inaongoza wafanyakazi 310 na wote wanahitaji kupata huduma wanazostahili ili wananchi wapate huduma ambazo nchi inafikiria kuzitoa kwao,” amesema.

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya  Tiba Shirikishi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delila Kimambo akieleza kazi zilizofanywa na kurugenzi yake  wakati wa kikao cha nne cha  baraza la wafanyakazi wa Taasisi hiyo  kilichofanyika leo jijini Dar es salaam. 
Wajumbe wa  Baraza la  Wafanyakazi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia mada ya sheria za kazi wakati wa kikao cha  nne  cha baraza hilo  kilichofanyika leo jijini Dar es salaam.Jumla ya wajumbe 59 walihudhuria kikao hicho.
Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha pamoja mara baada ya kumalizika kwa  kikao cha nne cha baraza la wafanyakazi wa Taasisi hiyo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. Waliokaa katikati ni Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi.  
 

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024