Posts

Showing posts from December, 2020

Yafahamu matibabu ya kibingwa ya magonjwa ya moyo yanayotolewa Taasisi y...

Image

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) yaombwa kufikisha uelewa wa magonjwa ya moyo mashuleni

Image
  Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Winnie Masakuya akitoa uelewa wa jinsi ya kutunza moyo ili uwe na afya njema kwa   walimu wakuu wa shule za Sekondari nchini waliofika katika banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupima viashiria vya magojwa ya moyo wakati wa mkutano wa walimu hao unaomalizika hivi karibuni   jijini Dodoma. Walimu wakuu wa shule za Sekondari nchini wameiomba Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kuhakikisha uelewa wa magonjwa ya moyo unatolewa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na siyo kwa watu wazima peke yao. Wamesema uelewa wa magonjwa hayo ukiwafikia wanafunzi utawasaidia kuitunza mioyo yao na hivyo kuweza kuishi maisha marefu zaidi tofauti na inavyofanyika kwa sasa ambapo uelewa unatolewa kwa watu wazima wengi wao wakiwa na umri wa kuanzia miaka 35 na kuendelea. Ombi hilo limetolewa hivi karibuni na baadhi ya walimu waliohudhuria mkutano wa 15 wa walimu wakuu wa shule za sekondari nchini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kik

Prof. Janabi awafundisha walimu wakuu wa shule za sekondari namna ya kue...

Image

Walimu nchini wapewa mbinu zitakazowawezesha kufaidi matunda ya uchumi wa kati katika miaka ijayo

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akitoa mada kuhusu magonjwa ya moyo na jinsi ya kuyaepuka kwa walimu waliohudhuria mkutano wa walimu wakuu wa shule za sekondari nchini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete uliopo jijini Dodoma. JKCI imeshiriki katika mkutano huo kwa kufanya upimaji wa viashiria vya magonjwa ya moyo  pamoja na kutoa uelewa (awareness) wa magojwa hayo. Na Veronica Mrema – Dodoma Walimu nchini wamepewa mbinu zitakazowawezesha kufaidi matunda ya uchumi wa kati katika miaka ijayo, miongoni mwa mambo muhimu waliyohimizwa kuyazingatia ni kutunza afya zao. Wamehimizwa pia kuepuka uzito uliokithiri na kufanya mara kwa mara uchunguzi wa afya ili kujua hali zao na kutibiwa mapema ikiwa watagundulika tayari wameanza kushambuliwa na magonjwa mbalimbali hususan yasiyoambukiza ambayo hivi sasa ni janga la dunia. Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa. Mohamed

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) yafanya upimaji wa viashiria vya magonjwa ya moyo pamoja na kutoa uelewa wa magojwa hayo katika mkutano wa walimu wakuu wa shule za sekondari nchini unaofanyika jijini Dodoma

Image
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akitoa mada kuhusu magonjwa ya moyo na jinsi ya kuyaepuka kwa walimu waliohudhuria mkutano wa walimu wakuu wa shule za sekondari nchini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete uliopo jijini Dodoma. JKCI imeshiriki katika mkutano huo kwa kufanya upimaji wa viashiria vya magonjwa ya moyo   pamoja na kutoa uelewa (awareness) wa magojwa hayo. Baadhi ya walimu wakuu wa shule za Sekondari nchini wakimsikiliza Prof. Mohamed Janabi wakati akitoa mada kuhusu magojwa ya moyo na jinsi ya kuyaepuka wakati wa   mkutano mkuu wa walimu hao uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete uliopo jijini Dodoma. JKCI imeshiriki katika mkutano huo kwa kufanya upimaji wa viashiria vya magonjwa ya moyo   pamoja na kutoa uelewa (awareness) wa magojwa hayo. Wafanyakazi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwapima walimu wakuu wa shule za Sekondari nchini viashiria vya magonjwa ya moyo wakati wa

Heart diseases services at Jakaya Kikwete Cardiac Institute, Tanzania

Image

Wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) waonesha huduma wanazozitoa kwa wagonjwa wanaowahudumia katika taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi wa mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee .

Image
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Agnes Lugendo akimweleza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Aboubakar Kunenge jinsi wauguzi wa Taasisi hiyo wanavyohudumia wagonjwa waliolazwa wodini wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi wa Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Karimejee. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amewapongeza Wauguzi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya ya kuokoa maisha ya wagonjwa jambo lililosaidia kupunguza vifo. Rc Kunenge alisema hayo hivi karibuni wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi wa Mkoa wa Dar es salaam yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee na kuwahimiza kuendelea kuchapa kazi kwa uwezo wao wote na kuwaahidi kwamba Serikali itaendelea kushirikiana nao bega kwa bega. Aidha RC Kunenge alisema anafurahi kuona hata zile kelele za wananchi kuhusu lugha chafu zimepungua na badala yake hivi sasa wauguzi wamekuwa na lugha ya upendo kwa wagonjwa jambo linalotia faraja