Wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) waonesha huduma wanazozitoa kwa wagonjwa wanaowahudumia katika taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi wa mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee .

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Agnes Lugendo akimweleza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Aboubakar Kunenge jinsi wauguzi wa Taasisi hiyo wanavyohudumia wagonjwa waliolazwa wodini wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi wa Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Karimejee.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amewapongeza Wauguzi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya ya kuokoa maisha ya wagonjwa jambo lililosaidia kupunguza vifo.

Rc Kunenge alisema hayo hivi karibuni wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi wa Mkoa wa Dar es salaam yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee na kuwahimiza kuendelea kuchapa kazi kwa uwezo wao wote na kuwaahidi kwamba Serikali itaendelea kushirikiana nao bega kwa bega.

Aidha RC Kunenge alisema anafurahi kuona hata zile kelele za wananchi kuhusu lugha chafu zimepungua na badala yake hivi sasa wauguzi wamekuwa na lugha ya upendo kwa wagonjwa jambo linalotia faraja.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa mkoa huo Dkt Rashid Mfaume aliwaahidi wananchi kutegemea mabadiliko makubwa katika sekta ya afya kwani Serikali ya mkoa imejidhatiti vizuri kutoa huduma bora na zenye tija. 

Afisa Uuguzi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rydness Mlashani  akimweleza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam Mhe. Aboubakar Kunenge jinsi wauguzi  wanaofanya kazi katika  maabara maalum ya kuchunguza na kutibu mishipa ya damu ya moyo (Catheterization laboratory - Cathlab) wanavyowahudumia wagonjwa wanaotibiwa katika maabara hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi wa mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika jana katika viwanja vya Karimjee  jijini Dar es Salaam.

Afisa Uuguzi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mahawa Asenga akimweleza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam Mhe. Aboubakar Kunenge jinsi wauguzi  wanaofanya kazi katika  vyumba vya upasuaji mkubwa wa moyo wanavyowahudumia wagonjwa kabla, wakati na baada ya kufanyiwa upasuaji  wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi wa mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika jana katika viwanja vya Karimjee  jijini Dar es Salaam.

Afisa Uuguzi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) aliyeko katika chumba cha wagonjwa walioko katika Uangalizi maalum (ICU) Verynice Issangya  akimweleza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam Mhe. Aboubakar Kunenge jinsi wauguzi  wanavyowahudumia wagonjwa waliotoka kufanyiwa upasuaji mkubwa na mdogo wa moyo na ambao hawajafanyiwa upasuaji  ila wanahitaji uangalizi maalum wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi wa mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika jana katika viwanja vya Karimjee  jijini Dar es Salaam.

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Marycelina Glandima aliyeko kliniki ya kuhudumia wagonjwa ambao hawajalazwa (OPD) akimweleza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam Mhe. Aboubakar Kunenge jinsi wauguzi  wanavyowapokea wagonjwa na kuhakikisha wamepata huduma za matibabu, dawa na vipimo wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi wa mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika jana katika viwanja vya Karimjee  jijini Dar es Salaam.

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari