Serikali imefunga mtambo wa kisasa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wenye thamani ya shilingi bilioni 4.6 wenye uwezo wa kufanya uchunguzi na matibabu ya moyo (Catheterization Laboratory - Cathlab) uliounganishwa na mtambo wa Carto 3 System 3D & mapping electrophysiology System ambao unauwezo wa kufanya uchunguzi na kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo
Serikali imefunga mtambo wa kisasa wenye thamani ya shilingi bilioni 4.6 wenye uwezo wa kufanya uchunguzi na matibabu ya moyo (Catheterization Laboratory - Cathlab) uliounganishwa na mtambo wa Carto 3 System 3D & mapping electrophysiology System ambao unauwezo wa kufanya uchunguzi na kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo. Fedha za kununuliwa kwa mtambo huo ambao umefungwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) zilitolewa na Serikali mwanzoni mwa mwaka jana. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi alisema mtambo huo umeshaanza kutumika, licha ya kutibu mfumo wa umeme wa moyo pia utafanya uchunguzi wa mishipa ya damu ya moyo, kuweka vifaa visaidizi vya moyo pamoja na kuzibua mishipa ya damu ya moyo iliyoziba. “Tunaishukuru Serikali kwa kuiwezesha JKCI na kufunga mtambo huu wa kisasa ambao unauwezo wa kuf...