Serikali imefunga mtambo wa kisasa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wenye thamani ya shilingi bilioni 4.6 wenye uwezo wa kufanya uchunguzi na matibabu ya moyo (Catheterization Laboratory - Cathlab) uliounganishwa na mtambo wa Carto 3 System 3D & mapping electrophysiology System ambao unauwezo wa kufanya uchunguzi na kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo
Fedha
za kununuliwa kwa mtambo huo ambao umefungwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) zilitolewa na Serikali mwanzoni mwa mwaka jana.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi alisema mtambo huo
umeshaanza kutumika, licha ya kutibu mfumo wa umeme wa moyo pia utafanya uchunguzi wa
mishipa ya damu ya moyo, kuweka vifaa visaidizi vya moyo pamoja na kuzibua
mishipa ya damu ya moyo iliyoziba.
“Tunaishukuru
Serikali kwa kuiwezesha JKCI na kufunga mtambo huu wa kisasa ambao
unauwezo wa kufanya uchunguzi na kutibu hitilafu
ya mfumo wa umeme wa moyo.Kufungwa kwa
mashine hii yenye teknlologia ya hali ya juu kutaweza kuokoa maisha ya watu
wengi wenye matatizo ya moyo ikiwemo mfumo wa umeme wa moyo hapa nchini ”,.
“Tuna
wagonjwa wengi ambao mfumo wa umeme wa moyo umekuwa haufanyi kazi vizuri hii
ikiwa ni pamoja na hitilamu ya mfumo wa
umeme wa moyo ambao mapigo yake ya moyo yanakwenda
haraka kuliko kawaida ambao tulikuwa
tunawasafirisha kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kutibiwa huku wengine wachache
wakipatiwa matibabu hapahapa nchini”, alisema Prof. Janabi.
Prof.
Janabi alisema mtu akiwa na tatizo
katika mfumo wa umeme wa moyo ambalo anaweza kulipata kwa kuzaliwa nalo au
athali ya ugonjwa linapelekea mfumo wa umeme wa moyo kubadili mapigo yake
inaweza kuwa chini ya 60 kwa dakika na
hivyo kusababisha mapigo kuwa chini sana au kuwa juu ya 100 kwa dakika na hivyo kuufanya moyo udunde kwa haraka. Kwa kawaida
mapigo ya moyo huwa ni 60 hadi 100 kwa dakika.
Mkurugenzi
huyo Mtendaji ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema kupitia
utaalam wanaoendelea kuupata kutoka kwa wenzao wa nchi za nje ambao wamewatangulia
katika matibabu ya moyo pamoja na
kusimikwa kwa mtambo huo wataweza kuwatibu wagonjwa hao hapa nchini
“Kwa
upande wa wataalamu tunao wa kutosha kwani kuna ambao tumewasomesha nchini
China na Afrika ya Kusini pia kupitia kambi mbalimbali za matibabu ya moyo
ambazo tunazifanya kwa kushirikiana na wenzetu wa nje ya nchi ambao wanautaalamu mkubwa zaidi
yetu kutatusaidia kupata utaalamu wa kutosha na wa kisasa”, alisema Prof.
Janabi.
Kwa
upande wake Hassan Ally kutoka kampuni ya Biosense webser ambao ndiyo wafungaji
wa mtambo huo alisema katika nchi za Afrika ya Mashariki mtambo huo ni wa pili
kufungwa hapa nchini ambapo mtambo wa kwanza ulifungwa katika Hospitali ya Aga
Khan iliyopo Mombasa nchini Kenya.
Alisema
mtambo huo una teknolojia mpya na ya kisasa ambayo hivi sasa inafanyika katika
matibabu ya moyo Duniani na kuzitaja nchi zingine ambazo zimefunga mtambo huo
katika bara la Afrika kuwa ni pamoja na Afrika ya Kusini na Misri.
“Tumeshatoa
na tutaendelea kutoa mafunzo kwa wataalamu wa Taasisi hii ili wajue jinsi ya kuutumia
mtambo huu na tutaendelea kutoa mafunzo
hayo kwa nchi zote za Afrika ambazo zimefunga mtambo huu wa kisasa ambao
unateknolojia mpya hapa Duniani”,
alisema Ally .
Naye
daktari
mwanamke pekee hapa nchini ambaye ni mtaalamu
mbobezi wa moyo na mzibuaji wa mishipa ya damu ya moyo wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Honoratha Maucky alisema kufungwa kwa mtambo huo
kutawasaidia kutoa huduma nyingi zaidi kwa wagonjwa na kuweza kuokoa maisha
yao.
Dkt. Maucky alisema tatizo la mfumo wa
umeme wa moyo ni moja ya magonjwa wanayokutana nayo kila siku hivyo basi kuwepo kwa mtambo
huo kutawasaidia kutoa huduma kwa wakati kwa wagonjwa wenye matatizo hayo.
“Teknolojia ya matibabu ya moyo
inakuwa kila siku kama mnavyoona tumefungiwa mtambo ambao unateknolojia mpya na
ya kisasa hivyo basi ni muhimu kwa
daktari kutenga muda wako ili uweze kujifunza kwa njia ya mtandao au kupitia
kwa wenzetu ambao wameendelea kimatibabu kuliko sisi kwa kufanya hivyo
hautakuwa nyuma ya teknolojia ya matibabu”, alisisitiza Dkt. Maucky.
Wataalamu wabobezi wa
moyo na wazibuaji wa mishipa ya damu ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimzibua mgonjwa mishipa miwili
ya damu ya moyo ambayo ilikuwa imeziba na kushindwa kupitisha damu vizuri.
Uzibuaji huo umefanyika kwa kutumia mtambo mpya wa kisasa wa (Catheterization Laboratory - Cathlab)
uliounganishwa na
mtambo wa Carto 3 System 3D & mapping electrophysiology System ambao Serikali umeununua kwa gharama ya shilingi bilioni 4.6.
Wataalamu wabobezi wa moyo na wazibuaji wa mishipa ya damu ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimzibua mgonjwa mishipa miwili ya damu ya moyo ambayo ilikuwa imeziba na kushindwa kupitisha damu vizuri. Uzibuaji huo umefanyika kwa kutumia mtambo mpya wa kisasa wa (Catheterization Laboratory - Cathlab) uliounganishwa na mtambo wa Carto 3 System 3D & mapping electrophysiology System wenye uwezo wa kufanya uchunguzi, kufunga vifaa visaidizi vya moyo, kuzibua mishipa ya damu ya moyo na kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo.
Comments
Post a Comment