Wafanyakazi bora wa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2020/21 wapongezwa

 


 Mkurugenzi wa kurugenzi ya Utawala na Fedha wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA Agness Kuhenga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kurugenzi hiyo mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora wa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2020/21. Wapili kushoto ni mfanyakazi aliyeshika nafasi ya pili Justina Lugali aliyetoka katika Kurugenzi hiyo na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni moja mfanyakazi bora wa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2020/21 aliyeshika nafasi ya tatu Theresia Tarimo wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora watatu iliyofanyika Leo katika Taasisi hiyo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti mfanyakazi bora wa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2020/21 aliyeshika nafasi ya pili Justina Lugali wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora watatu iliyofanyika Leo katika Taasisi hiyo. Mfanyakazi huyo pia amepewa kiasi cha shilingi milioni moja na laki tano


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni mbili mfanyakazi bora wa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2020/21 aliyeshika nafasi ya kwanza Khalifa Abdalla wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora watatu iliyofanyika Leo katika Taasisi hiyo.

Pacha na: JKCI

Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Maabara ya JKCI yapata ithibati ya kimataifa (ISO 15189:2012)