Wajumbe wa bodi ya zabuni na wafanyakazi wa kitengo cha Ununuzi na Ugavi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wapewa mafunzo ya Sheria ya Ununuzi wa Umma na kanuni zake
Mkurugenzi wa Kujenga Uwezo na
Ushauri wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Mhandisi Mary Swai akizungumza
na wajumbe wa bodi ya zabuni na watumishi wa kitengo cha Ununuzi na Ugavi wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mafunzo ya siku nne ya Sheria
ya Ununuzi wa Umma na kanuni zake yaliyotolewa kwa wafanyakazi wa Taasisi hiyo.
Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
Baadhi ya wajumbe wa bodi ya zabuni
na watumishi wa kitengo cha Ununuzi na Ugavi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa wakati wa mafunzo ya siku nne ya
Sheria ya Ununuzi wa Umma na kanuni zake.
Afisa Ununuzi wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Leah Komba akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji
wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi mara baada ya kuhitimu mafunzo ya siku nne
ya Sheria ya Ununuzi wa Umma na kanuni zake yaliyotolewa na Mamlaka ya udhibiti
wa ununuzi wa umma (PPRA) kwa wajumbe wa bodi ya zabuni na watumishi wa kitengo
cha Ununuzi na Ugavi wa Taasisi hiyo.
Mhasibu wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya zabuni ya JKCI Reuben Nyiti akipokea
cheti kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi mara baada
ya kuhitimu mafunzo ya siku nne ya Sheria ya Ununuzi wa Umma na kanuni zake
yaliyotolewa na Mamlaka ya udhibiti wa ununuzi wa umma (PPRA) kwa wajumbe wa
bodi ya zabuni na watumishi wa kitengo cha Ununuzi na Ugavi kwa wafanyakazi wa Taasisi
hiyo.
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo
kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya
zabuni ya JKCI Godwin Sharau akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi mara baada ya kuhitimu mafunzo ya siku nne ya
Sheria ya Ununuzi wa Umma na kanuni zake yaliyotolewa na Mamlaka ya udhibiti wa
ununuzi wa umma (PPRA) kwa wajumbe wa bodi ya zabuni na watumishi wa kitengo
cha Ununuzi na Ugavi wa Taasisi hiyo.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Mary Haule ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya zabuni ya JKCI
akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed
Janabi mara baada ya kuhitimu mafunzo ya siku nne ya Sheria ya Ununuzi wa Umma
na kanuni zake yaliyotolewa na Mamlaka ya udhibiti wa ununuzi wa umma (PPRA)
kwa wajumbe wa bodi ya zabuni na watumishi wa kitengo cha Ununuzi na Ugavi wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na
wajumbe wa bodi ya zabuni na watumishi wa kitengo cha Ununuzi na Ugavi wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) baada ya kumalizika kwa mafunzo ya siku
nne ya Sheria ya Ununuzi wa Umma na kanuni zake. Wapili kulia waliokaa ni Mkurugenzi
wa Kujenga Uwezo na Ushauri wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA)
Mhandisi Mary Swai.
Comments
Post a Comment