Posts

Showing posts from November, 2021

UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE

Image
 

Maktaba ya watoto Hospitalini itawajenga kupenda kusoma kuliko kuogopa matibabu

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimwelezea namna taasisi hiyo inavyofanya kazi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi alipofanya ziara katika taasisi hiyo jana kwa ajili ya kuangalia huduma zinazotolewa. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi akimjulia hali mtoto aliyelazwa katika wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo wakati wa ziara yake ya kutembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jana kwa ajili ya kuangalia huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo . Daktari bingwa wa wagonjwa waliolazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Vivian Mlawi akimwelezea Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi namna ambavyo wanatoa huduma ya uangalizi maalum kwa watoto waliolazwa katika chumba hicho wakati alipofanya ziara ya kutembelea taasisi hiyo kwa ajil

Mpango mkakati wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kwa kipindi cha miaka mitano ijayo ni kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akifunga kikao cha viongozi wa taasisi hiyo kwa ajili ya kutoa maoni juu ya rasimu ya mpango mkakati wa pili wa utendaji kazi wa Taasisi hiyo utakaotumika kwa kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha 2022/23 Jana Jijini Dar es Salaam Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni miongoni mwa wanakamati wa rasimu ya mpango mkakati Pedro Pallangyo akielezea baadhi ya vitu vilivyopo katika rasimu ya mpango mkakati wa pili wa utendaji kazi wa Taasisi hiyo wakati wa kikao cha kutoa maoni juu ya rasimu ya mpango mkakati huo utakaotumika kwa kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha 2022/23 Jana Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA Agnes Kuhenga akitoa ufafanuzi wakati wa kikao cha kutoa maoni juu ya rasimu ya mpango mkakati wa pili wa utendaji kazi wa Taasisi hiyo utakaotumika kwa kipindi cha miaka mitano ijayo

Madaktari wazawa wabadilisha mshipa wa damu uliotanuka na Valvu yake

Image
  Madaktari wazawa mabingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kubadilisha mshipa mkubwa wa damu (aorta) uliokuwa umetanuka pamoja na valvu yake (Aortic valve insufficiency) bila ya usimamizi wa madaktari kutoka nje baada ya miaka kadhaa ya kujifunza upasuaji huo kutoka kwa wataalam wenzao wanaofika JKCI kwa ajili ya kubadilishana uzoefu. ********************************************************************************************************************************************** Kwa mara ya kwanza madaktari wazawa mabingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wamefanya upasuaji wa kubadilisha mshipa mkubwa wa damu (Aorta) uliokuwa umetanuka pamoja na valvu yake (Aortic valve insufficiency) bila ya usimamizi wa madaktari kutoka nje baada ya miaka kadhaa ya kujifunza upasuaji huo kutoka kwa wataalam wenzao wanaofika JKCI kwa ajili ya kubadilishana uzoefu. Upasuaji huo

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MAFANIKIO YA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KWA MIAKA 60 YA UHURU WA TANZANIA BARA.

  Ndugu Wanahabari, Disemba 2021 nchi yetu inaadhimisha miaka 60 ya Uhuru tangu tarehe 09 Desemba, 1961 tulipoanza kujitawala hivyo, maadhimisho haya ni tofauti na miaka mingine kutokana na haja ya kutafakari kwa pamoja tulikotoka, tulipo na tunakoelekea. Maadhimisho haya yanaongozwa na Kaulimbiu isemayo “MIAKA 60 YA UHURU; TANZANIA IMARA, KAZI IENDELEE”. Tangu mwaka 1961, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekuwa ikitekeleza Sera, Miongozo na Sheria mbalimbali kulingana na maboresho ya muundo wa wizara kwa wakati husika. Kufikia mwaka 2016 Wizara mbili ziliunganishwa ambazo ni Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, hivyo kutengeneza Idara Kuu ya Afya inayoshughulikia masuala yote ya Afya na Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii inayoshughulikia Masuala yote ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee, Watoto na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali. Ndugu Wanahabari, huduma za tiba ya magonjwa pamoja na maendeleo ya jamii