Mpango mkakati wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kwa kipindi cha miaka mitano ijayo ni kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi
Mkuu
wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Daniel
Bunare akichangia hoja wakati wa kikao cha kutoa maoni juu ya rasimu ya mpango
mkakati wa pili wa utendaji kazi wa Taasisi hiyo utakaotumika kwa kipindi cha
miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha 2022/23 Jana Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi hiyo na wanakamati wa rasimu ya mpango mkakati wa pili wa utendaji kazi wa Taasisi hiyo baada ya kikao cha kutoa maoni juu ya rasimu ya mpango mkakati huo utakaotumika kwa kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha 2022/23 Jana Jijini Dar es Salaam
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Wakurugenzi wa Idara na wakuu wa vitengo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kuwa mfano wa kuigwa na hospitali nyingine nchini pamoja na watumishi wanaowaongoza kwa kutekeleza majukumu yao kulingana na mpango mkakati wa utendaji kazi wa taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Kutekeleza
kwao mpango mkakati huo kutasaidia kuboresha huduma za matibabu ya
moyo na kuweza kutoa huduma zote za kibingwa za magonjwa hayo hapa nchini.
Rai
hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati wa kikao cha viongozi hao kilichofanyika
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa maoni juu ya rasimu
ya mpango mkakati wa pili wa utendaji kazi wa Taasisi hiyo utakaotumika
kwa kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha ujao wa 2022/23.
Prof.
Janabi alisema rasimu ya mpango mkakati huo wa kazi imeeleza kazi ambazo kila
idara na kitengo zinatakiwa kufanya na imewashirikisha wafanyakazi wote kwa
ajili ya kuweka maoni yao lakini pia rasimu hiyo imeandaliwa na baadhi ya
wafanyakazi wa JKCI jambo ambalo litarahisisha utendaji kazi wa Taasisi hiyo.
“Nimefurahishwa
na viongozi wote kwa pamoja jinsi mlivyoshirikiana kuweka mawazo yenu katika
kuboresha rasimu hii ya kwanza ya mpango mkakati itakayoanza kutumika mwaka
2022/2023 hadi mwaka 2026/2027 tukiwa na lengo la kuendelea kuboresha huduma
zetu lakini pia kutoka hapa tulipo na kuweza kutoa huduma zote za kibingwa za
magonjwa ya moyo”,.
“Mpango
mkakati huu ukianza kutumika ni vyema tukajiwekea malengo kwamba kila jukumu
lililowekwa linafanyika kwa wakati husika na kumalizika kwa wakati kwa
kufanya hivyo ninahakika baada ya miaka mitano ijayo tutakuwa tumefikia malengo
yetu kwa asilimia mia moja”, alisema Prof. Janabi
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Fedha na Mipango CPA Agnes Kuhenga aliwashukuru
wanakamati walioandaa rasimu hiyo ya mpango mkakati wa pili kwa mawazo na maoni
yao ambayo yameweza kutoa rasimu inayokidhi vigezo vya kada zote zilizopo
katika taasisi hiyo.
“Mpango
mkakati huu utakapokamilika na kuanza kutumika bado utaendelea kupitiwa mara
kwa mara ili yale yaliyoainishwa yaweze kufanyika kwa vitendo na hivyo
kuboresha zaidi huduma tunazozitoa katika Taasisi yetu",.
“Leo
katika kikao hiki cha kupitia rasimu ya kwanza ya mpango mkakati wa pili wa
utendaji kazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete tumechukua tena mawazo ya
viongozi walioshiriki kikao hiki ambayo tutaenda kuyafanyia kazi katika
kuboresha rasimu hii na kutoa rasimu ya pili”, alisema CPA Agnes.
Naye
Mkuu wa Kitengo cha Mipango wa Taasisi hiyo Vida Mushi alisema kushirikishwa
kwa watendaji katika uandaaji wa mpango mkakati wa utendaji kazi za kila siku
kunamsaidia mtumishi kutekeleza majukumu yake kirahisi kwani anakuwa na ufahamu
wa nini anatakiwa kufanya.
“Kushirikishwa
kwangu kuandaa mpango mkakati huu na kutoa maoni yangu kutaturahisishia mimi na
wafanyakazi wenzangu kutekeleza majukumu yetu ya kila siku kwasababu
kumenipa ufahamu mkubwa hivyo itakua rahisi pale ufuatiliaji na tathmini utakapofanyika”,
alisema Vida.
Comments
Post a Comment