Jamii yatakiwa kuchunguza afya mara kwa mara ili kuzuia magonjwa yasiyoambukiza
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Edward Martin akiwafundisha wafanyakazi wa TATA Africa Holdings Limited umuhimu wa kupata vipimo na matibabu ya magonjwa ya moyo mapema wakati wa kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya moyo iliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo vingunguti Dar es Salaam. Fundi sanifu wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikiwete (JKCI) Renata Kulwa akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography - ECHO) mfanyakazi wa TATA Africa Holdings Limited wakati wa kambi maalum ya uchunguzi na matibabu ya moyo iliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo vingunguti Dar es Salaam. Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji akimfundisha namna ya kuzingatia lishe bora mfanyakazi wa TATA Africa Holdings Limited wakati wa kambi maalum ya uchunguzi na matibabu ya moyo iliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo vingunguti Dar es Salaam. Baadhi ya wafanyakazi wa TATA Africa...