Hakikisheni huduma za matibabu ya moyo za kibingwa zinawafikia wananchi walioko vijijini – Mhe. Nyongo
Kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya Jamii imeitaka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kuhakikisha huduma za matibabu ya moyo za kibingwa wanazozitoa zinawafikia wananchi walioko vijijini. Agizo hilo limetolewa jana na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Stanslaus Nyongo wakati akizungumza na menejimenti ya Taasisi hiyo mara baada ya kumaliza ziara ya kukagua matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali kama zinatumika ipasavyo pamoja na kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa. Mhe. Nyongo ambaye pia ni Mbunge wa Maswa Mashariki alisema kamati yake imeridhishwa na huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo na kuishukuru Serikali kwa kuanzisha kituo hicho kinachotoa huduma za kimataifa ambacho kimekuwa mkombozi na kuwasaidia watu wengi wakiwemo watanzania na wasio watanzania. Alisema huko vijijini kuna watu wakiwemo watoto wanamatatizo ya moyo ni vyema nao wakapata huduma za matibabu hayo ambazo hivi sasa zinapatikana hapa nchini. Pia wa...