Wachezaji 24 wa Timu ya Serengeti Boys wapimwa vipimo vya Moyo
Mtaalam kutoka Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Nuru Lugawa akimpima uzito na urefu mchezaji wa
timu ya taifa chini ya miaka 17 Serengeti Boys Mohamed Mbarak wakati wachezaji
wa timu hiyo walivyofika JKCI kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya ya moyo
kabla ya kushiriki mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON)
yatakayofanyika nchini Morocco katikati ya mwezi mwezi huu.

Afisa Uuguzi wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Gudila Swai akimpima shinikizo la damu
mchezaji wa timu ya taifa chini ya miaka 17 Serengeti Boys Silverster Otto
wakati wachezaji wa timu hiyo walipofika JKCI kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi
wa magonjwa ya moyo kabla ya kushiriki mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika
(AFCON) yatakayofanyika nchini Morocco katikati ya mwezi huu.
Fundi sanifu wa moyo
(Cardiovascular technologist) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jasmin
Keria akimpima mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiography –
ECG) kapteni wa timu ya taifa chini ya miaka 17 Serengeti Boys Ladaki
Chasambi wakati timu hiyo ilipofika JKCI kwa ajili ya kuwafanyiwa uchunguzi wa
magonjwa ya moyo kabla ya kushiriki mashindano ya kombe la Mataifa ya
Afrika (AFCON) yatakayofanyika nchini Morocco katikati ya mwezi huu.
Baadhi ya wachezaji
wa timu ya taifa chini ya miaka 17 Serengeti Boys wakisubiri kufanyiwa
uchunguzi wa magonjwa ya moyo leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Wachezaji 24 wa timu hiyo walifanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo
unavyofanya kazi, umeme wa moyo unavyofanya kazi na damu ikiwa ni mojawapo ya
kutekeleza sheria ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa kila
mchezaji anayeshiriki mashindano hayo kupima.
Comments
Post a Comment