Posts

Showing posts from May, 2021

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) yanunua mashine mbadala ya mapafu na moyo (Heart lung machine) itakayotumika wakati wa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo yenye thamani ya shilingi 383,596,000/=.

Image
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) David Wapalila akiwa ameishika mashine mbadala ya mapafu na moyo (Heart lung machine) itakayotumika   wakati wa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo. Mashine hiyo ya kisasa yenye thamani ya shilingi   383,596,000/= imenunuliwa na Taasisi hiyo kwa ajili ya kuboresha huduma za upasuaji wa moyo. JKCI ina jumla ya mashine za aina hiyo nne. Picha ya mashine mbadala ya mapafu na moyo (Heart lung machine) itakayotumika   wakati wa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo ambayo  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeinunua  kwa thamani ya shilingi    383,596,000/=  kwa ajili ya kuboresha huduma za upasuaji wa moyo. 

Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Gwajima afanya kikao na viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa ajili ya kuangalia namna ya kuboresha huduma zinazotolewa kwa wanachama wa NHIF

Image
Waziri wa Afya,   Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)   wakati wa kikao alichokiitisha jana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia namna ya kuboresha huduma zinazotolewa kwa wanachama wa mfuko wa   NHIF wanaotibiwa katika Hospitali hizo za Taifa. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma ya Uuguzi wa JKCI RN Robert Mallya. Mkurugenzi wa Tiba na huduma za kitabibu kutoka mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Dkt. David Mwanesano akielezea kuhusu huduma za matibabu zinazolipiwa kwa wanachama wa mfuko huko wakati wa kikao kilichoitishwa na Waziri wa Afya,    Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima kwa     viongozi wa NHIF, Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI),Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa ajili ya kuangalia namna ya kubore

Waagizaji na wasambazaji wa dawa za binadamu za moyo waahidi kuendelea kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ili wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo wapate dawa kwa wakati

Image
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na waagizaji na wasambazaji wa dawa za binadamu za moyo mara baada ya kumalizika kwa  mkutano baina yao ambao ulijadili changamoto zinazowakabili na jinsi ya kuzitatua ikiwa ni  kuboresha upatikana wa dawa kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Mkutano huo ulifanyika hivi karibuni katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Uongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) umekutana   na waagizaji na wasambazaji wa dawa za binadamu za moyo ili kujua changamoto zinazowakabili na jinsi ya kuzitatua ikiwa ni   kuboresha upatikana wa dawa kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Kikao hicho cha wadau hao   kilifanyika hivi karibuni katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam ambapo wawakilishi zaidi ya 30 kutoka kampuni mbalimbali za dawa walihudhuria. Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya K

Serikali yafunga mtambo wa kutibu mfumo wa umeme wa moyo katika Taasisi ...

Image

Wachezaji 16 wa Timu ya Taifa ya Ufukweni (Beach Soka) wafanyiwa uchunguzi wa Moyo na Mapafu

Image
Mtaalam wa Maabara wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jesca Mlay akimtoa damu mchezaji wa timu ya taifa ya ufukweni (Beach Soka) Shabani Kodo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya ya mwili wakati wachezaji 16 wa timu hiyo walipofika katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya ya moyo kabla ya kushiriki mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yatakayofanyika nchini Senegal tarehe 23 hadi 30 Mei mwaka huu. Radiografa wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Shaniath Mzirai akimpima X-ray ya kifua kuchunguza moyo na mapafu mchezaji wa timu ya taifa ya ufukweni (Beach Soka) Kashiru Salum kwa kutumia mashine ya X-ray wakati  wachezaji 16 wa timu hiyo walipofika katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya ya moyo kabla ya kushiriki mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yatakayofanyika nchini Senegal tarehe 23 hadi 30 Mei mwaka huu.   Fundi sanifu wa moyo (Cardiovascular technologist) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)   Gerson Mp

Fahamu shinikizo lako la damu,uepukane na kifo cha ghafla kinachoweza kutokana na magonjwa ya moyo

Image

Watu 204 wamefanyiwa upimaji wa magonjwa ya moyo bila malipo katika maadhimisho ya siku ya Shinikizo la Juu la Damu Duniani

Image
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Joseph Katoto akimpima urefu na uzito mkazi wa Mbezi Luis wakati wa upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wakazi wa Wilaya ya Ubungo na vitongoji vyake katika kuadhimisha siku ya Shinikizo la Juu la Damu Duniani jana katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam. Jumla ya wananchi 204 wamefanyiwa upimaji wa magonjwa ya moyo bila malipo. Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Grace Sanga akimpima wingi wa sukari mwilini mkazi wa Ubungo wakati wa upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wakazi wa Wilaya ya Ubungo na vitongoji vyake katika kuadhimisha siku ya Shinikizo la Juu la Damu Duniani jana katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam. Jumla ya wananchi 204 wamefanyiwa upimaji wa magonjwa ya moyo bila malipo. Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji na mwenzake kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Mosile wakitoa ushauri wa lishe bora kwa mkazi wa Wil

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na uongozi wa wilaya ya Ubungo watafanya upimaji wa magonjwa ya Moyo bila malipo kwa wananchi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake tarehe 17/5/2021 ikiwa ni siku ya maadhimisho ya siku ya Shinikizo la juu la Damu Duniani.

Image
                                        Mwananchi akipimwa Shinikizo la Damu (BP)  

Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) washiriki futari ya pamoja iliyoandaliwa na Kurugenzi ya Tiba Shirikishi

Image
Mfanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete  (JKCI) Fathiya Mustafa akiomba dua ya chakula wakati wa futari iliyoandaliwa na Kurugenzi ya Tiba Shirikishi jana Jijini Dar es Salaam. Kila mwaka wakati wa Ramadhani Kurugenzi tano za Taasisi hiyo zinaandaa futari kwa nyakati tofauti kwa ajili ya wafanyakazi wa Taasisi hiyo Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete  (JKCI) wakichukua chakula wakati wa futari ya pamoja iliyoandaliwa na Kurugenzi ya Tiba Shirikishi jana Jijini Dar es Salaam. Kila mwaka wakati wa Ramadhani Kurugenzi tano za Taasisi hiyo zinaandaa futari kwa nyakati tofauti kwa ajili ya wafanyakazi wa Taasisi hiyo  Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete  (JKCI) wakila futari iliyoandaliwa na Kurugenzi ya Tiba Shirikishi jana Jijini Dar es Salaam. Kila mwaka wakati wa Ramadhani Kurugenzi tano za Taasisi hiyo zinaandaa futari kwa nyakati tofauti kwa ajili ya wafanyakazi wa Taasisi hiyo  

Fahamu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo ambapo mapigo yanakwenda haraka kuliko kawaida (Tachyarrhythmia’s)

Image

Ongezeko la mstuko wa moyo "Heart Attack" katika kipindi hiki cha mwezi ...

Image

Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) washiriki futari ya pamoja iliyoandaliwa na Kurugenzi ya Magonjwa ya Moyo

Image
  Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakichukuwa chakula wakati wa futari ya pamoja iliyoandaliwa na Kurugenzi ya Magonjwa ya Moyo jana jijini Dar es Salaam. Kila mwaka wakati wa mwezi wa mfungo wa Ramadhan Kurugenzi tano za Taasisi hiyo zinaandaa futari kwa nyakati tofauti kwa ajili ya wafanyakazi wa Taasisi hiyo. Futari hiyo ilidhaminiwa na kampuni ya Samiro ambao ni waagizaji na wasambazaji wa dawa za binadamu.   Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakila   futari iliyoandaliwa na Kurugenzi ya Magonjwa ya Moyo jana jijini Dar es Salaam. Kila mwaka wakati wa mwezi wa mfungo wa Ramadhan Kurugenzi tano za Taasisi hiyo zinaandaa futari kwa nyakati tofauti kwa ajili ya wafanyakazi wa Taasisi hiyo. Futari hiyo ilidhaminiwa na kampuni ya Samiro ambao ni waagizaji na wasambazaji wa dawa za binadamu.   Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Magonjwa ya Moyo ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo Tatizo Waane akila futari huku akibadilishana mawazo na  A

Sababu ya ongezeko la mstuko wa moyo “heart attack” katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan duniani

Image
Profesa Mohamed Janabi MD.,PhD.   Katika mwezi huu wa Ramadhan familia nyingi nchini na duniani kwa jumla kuna   nchi ambazo   raia wake wanafunga   saumu hii tukufu kama nguzo moja kati ya tano za kiislaam. Chakula cha jioni au kama kinavyojulikana IFTAR/FUTARI mbali ya kuwa na aina mbali mbali za vyakula bali pia huwa ni vingi kuliko siku za kawaida.   Kula futari nyingi kipindi cha magharibi sio tu kutafanya wafungaji na waalikwa wengine kuongezeka uzito mwezi huu wa Ramadhan bali kwa wa wale walaji   ambao wana matatizo mbali mbali ya moyo kama shinikizo la damu la juu (High Blood Pressure), moyo dhaifu (heart failure), moyo uliopanuka (Dilated Cardiomyopathy), mishipa/mirija ya moyo iliyoziba (coronary artery disease CAD)   wanaweza kupata matatizo ya kiafya .     Ulaji wa chakula   kingi kunaweza kuchochea mstuko wa ghafla wa moyo   (trigger heart attack).   Mstuko wa moyo unasababisha mamilioni ya watu kupoteza maisha kila mwaka duniani.   Kila mwaka vifo hivi vinaongezeka z