Wauguzi watakiwa kupunguza matumizi ya simu wanapowahudumia wagonjwa


Afisa Uuguzi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya (JKCI) Joshua Ogutu ambaye ni mratibu wa mafunzo ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi (Critical Care Emergence) akizungumza wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa mafunzo hayo  kwa wauguzi 12 kutoka Hospitali mbalimbali nchini.

Washiriki wa mafunzo ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi (Critical Care Emergence) yanayotolewa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi wakati akifungua kozi hiyo ya wiki 27 inayotolewa kwa wauguzi kutoka Hospitali mbalimbali nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi  akifungua mafunzo ya wiki 27 ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi (Critical Care Emergence)  yanayotolewa katika Taasisi hiyo  kwa wauguzi 12 kutoka Hospitali mbalimbali nchini.

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akizungumza na washiriki wa mafunzo ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi (Critical Care Emergence)  wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa mafunzo hayo kwa wauguzi 12 kutoka Hospitali mbalimbali nchini iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. 

 Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Mfunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge  akizungumza na washiriki wa mafunzo ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi (Critical Care Emergence)  wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa mafunzo hayo  kwa wauguzi 12 kutoka Hospitali mbalimbali nchini iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.  

 Afisa Uuguzi kutoka Hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando Archileus Dominick ambaye ni mshiriki wa mafunzo ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi (Critical Care Emergence) yanayotolewa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akitoa neno la shukrani wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo jijini Dar es Salaam.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki 12 wa mafunzo ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi (Critical Care Emergence) yanayotolewa katika Taasisi hiyo. Mafunzo hayo ya wiki 27  yanatolewa kwa wauguzi kutoka Hospitali mbalimbali nchini. 

****************************************************************************************************************************************************************

Wauguzi wanaofanya kazi katika wodi za wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU) pamoja na wodi zingine wametakiwa kutokutumia simu muda mwingi wawapo kazini kwani mazingira yao ya kazi yanawataka kuwa karibu na wagonjwa wanaowahudumia kutokana na maisha yao kuwa hatarini.

Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati akifungua mafunzo  ya wiki 27 ya  jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi (Critical Care Emergence) yanayotolewa na Taasisi hiyo kwa wauguzi kutoka Hospitali mbalimbali nchini.

Prof. Janabi alisema katika watumishi wa afya wauguzi ndiyo wanaokaa na wagonjwa muda mrefu wodini na vifo vingi vya wagonjwa vinatokea huko,  hivyo basi watumie muda wa kazi vizuri  kwa kutoa huduma bora kwa wagonjwa kwa kufanya kila kinachotakiwa ili kuokoa maisha yao na iwe ni bahati mbaya mgonjwa amefariki.

“Unapokuwa kazini tumia muda mwingi kutoa huduma kwa mgonjwa na siyo kutumia simu, haikatazwi kuongea na simu pale utakapopigiwa  simu ya umuhimu pokea au kutumiwa ujumbe wa umuhimu ujibu,  kama ni kutumia simu kwa mawasiliano ya kawaida utayafanya  baada ya muda wa kazi”,.

“Ukisikia mashine ya cardiac monitor ambayo inafanya uangalizi wa karibu kwa wagonjwa mahututi inalia usipuuze fahamu kuwa kuna kitu hakiko sawa nyanyuka mahali ulipo nenda kamuangalie mgonjwa kama yuko salama,  ukikuta yuko salama angalia mashine ina shida gani”, alisistiza Prof. Janabi.

Mkurugenzi huyo Mtendaji ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo  alisema Taasisi hiyo kutokana na huduma inazozitoa ikiwemo ya upasuaji wa moyo iliona kuna uhitaji wa kuwa na wataalamu wa kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi na kuamua kuwasomesha wataalamu wake kozi hiyo  nje ya nchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uuguzi ambao ndiyo waandaaji wa kozi hiyo Robert Mallya alisema wazo la kufundisha mafunzo hayo  lilikuja baada ya Serikali kuzihamishia hospitali zote za mikoa katika  wizara ya Afya na kuhakikisha hospitali hizo zinakuwa na ICU ambazo zitatoa huduma ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi. Kutokana na uhitaji uliopo wakaona kuna haja ya kuanzisha kozi hiyo ili wabadilishane ujuzi  walionao nao na wauguzi wengine nchini.

Mallya alisema kozi hiyo inatolewa kwa mara ya kwanza katika Taasisi hiyo baada ya  kumalizika kwa kozi hiyo watatangaza nyingine ili wale wanaotaka kusoma nao wapate nafasi ya kusoma na kuwataka washiriki wa kozi hiyo pindi watakapomaliza na kurudi  katika maeneo yao ya kazi walete mabadiliko ya utoaji wa huduma katika Hospitali walizotoka.

“Uhitaji wa utaalamu huu ni mkubwa sisi tunawaandaa ili muweze kutoa huduma hii kwa wagonjwa wa ICU tumieni miezi sita kujifunza ili mtakapomaliza mkatoe huduma kwa wagonjwa, kuwafundisha wenzenu na kuwa mabalozi wazuri.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake wa kozi hiyo Afisa Uuguzi kutoka Hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando Archileus Dominick alisema watautumia muda vizuri katika kujifunza na anaamini watajifunza mambo mengi ambayo yatawasaidia katika kazi zao za kila siku za kuwahudumia wagonjwa.

Washiriki wa kozi hiyo ambao wako 12 watajifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na jinsi ya kumuhudumia mgonjwa aliyepo katika mashine ya kumsaidia kumpumua (Ventilator)na jinsi ya kutumia mashine hiyo. Jinsi ya kutumia mashine ya Cardiac Monitor ambayo inafanya uangalizi wa karibu kwa wagonjwa mahututi, kuustua moyo ulioacha kufanya kazi (Defibrillation).

Pia watajifunza matumizi ya mashine inayosafisha damu ya mgonjwa wa figo na jinsi ya kumuhudumia mgonjwa anayehitaji huduma ya dharula,  jinsi ya kutoa tiba maalum za wagonjwa wa figo, kutoa dawa za wagonjwa wa moyo na jinsi ya kumuhudumia mgonjwa ambaye moyo wake haufanyi kazi vizuri (Basic Life Support – BLS, Advanced Cardiac Life Support – ACLS).


Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari