Wananchi 437 wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo na kisukari ambapo asilimia 60 wamekutwa na matatizo
Mwananchi wa Halmashauri ya Chalinze akisoma jarida la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa upimaji maalum unliofanywa kwa wananchi hao kwa ajili ya kuchunguza magonjwa ya moyo na kisukari katika Hopitali ya Halmashauri hiyo iliyopo Msoga wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. Afisa kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Aliston Jovin akiwagawia vipeperushi vinavyoelezea huduma za matibabu zinazotolewa na JKCI wananchi waliofika katika Hospitali ya Halmashauri ya Chalinze iliyopo Msoga kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo uliofanywa na wataalam wa moyo kutoka JKCI katika Halmashauri hiyo iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. Afisa Uuguzi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rahabu Tamba akimpima urefu na uzito mwananchi aliyefika katika Hospitali ya Halmshauri ya Chalinze iliyopo Msoga wilayani Bagamoyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo uliokua ukifanywa na wataalam wa moyo kutoka JKCI kwa wananchi wa Chalinze. Dakta...