Wataalamu wa moyo waongezewa ujuzi wa jinsi ya kufanya kipimo cha kuangalia moyo unavyofanya kazi kwa kutumia mashine ya Echocardiogram (ECHO).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane akizungumza na washiriki wa mafunzo ya upimaji wa moyo wa kuchunguza wagonjwa ambao mioyo yao imeshindwa kufanya kazi vizuri kwa kutumia mashine ya Echocardiogram yaliyotolewa na kampuni ya usambazaji wa mashine za Echo ya Mindray iliyopo nchini China. Mafunzo hayo yalitolewa jana katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Meneja mfumo wa picha za matibabu kutoka kampuni ya usambazaji wa mashine za Echo ya Mindray iliyopo nchini China Li Li akiwafundisha madaktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) namna ya kuwachunguza wagonjwa ambao mioyo yao imeshindwa kufanya kazi vizuri kwa kutumia mashine ya Echocardiogram wakati wa mafunzo maalum ya siku moja yaliyotolewa kwa madaktari.
Baadhi ya Madaktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) wakifuatilia mafunzo ya namna ya kuwachunguza wagonjwa ambao
mioyo yao imeshindwa kufanya kazi vizuri yaliyokuwa yakitolewa na Meneja mfumo
wa picha za matibabu kutoka kampuni ya usambazaji wa mashine za Echocardiogram (ECHO)
ya Mindray iliyopo nchini China Li Li (hayupo pichani) wakati wa mafunzo maalum
yaliyotolewa kwa madaktari hao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi
hiyo jana Jijini Dar es Salaam.
Mtaalam wa Radiolojia kutoka nchini Somalia
Dkt. Hassan Abdinur akiwafundisha madaktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) namna ya kuwachunguza wagonjwa ambao mioyo yao imeshindwa kufanya kazi vizuri
kwa kutumia mashine ya Echocardiogram (ECHO) yaliyotolewa na kampuni ya
usambazaji wa mashine za ECHO ya Mindray iliyopo nchini China. Mafunzo hayo
yalitolewa jana katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es
Salaam.
Mtaalam wa Radiolojia kutoka nchini Somalia
Dkt. Hassan Abdinur akiwafundisha madaktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) namna ya kuwachunguza wagonjwa ambao mioyo yao imeshindwa kufanya kazi vizuri
kwa kutumia mashine ya Echocardiogram (ECHO) yaliyotolewa na kampuni ya
usambazaji wa mashine za ECHO ya Mindray iliyopo nchini China. Mafunzo hayo
yalitolewa jana katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es
Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo na Utafiti wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akitoa neno la
shukrani baada ya kumalizika kwa mafunzo ya upimaji wa moyo wa kuchunguza
wagonjwa ambao mioyo yao imeshindwa kufanya kazi vizuri kwa kutumia mashine ya
Echocardiogram (ECCHO) yaliyotolewa na kampuni ya usambazaji wa mashine za Echo
ya Mindray iliyopo nchini China. Mafunzo hayo ya siku moja yalitolewa jana
katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Madaktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) ambao ni washiriki wa mafunzo ya upimaji wa moyo wa kuchunguza wagonjwa
ambao mioyo yao imeshindwa kufanya kazi vizuri kwa kutumia mashine ya
Echocardiogram (ECHO) yaliyotolewa na kampuni ya usambazaji wa mashine za ECHO
ya Mindray iliyopo nchini China wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
kumalizika kwa mafunzo hayo jana jijini Dar es Salaam.
Dar es Salaam Madaktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo 28 kutoka
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao watatu kutoka Hospitali ya
Rabininsia na Saifee zilizopo jijini Dar es Salaam wameshiriki mafunzo ya siku
moja upimaji wa moyo unavyofanya kazi kwa
kutumia mashine ya Echocardiogram (ECHO) yaliyotolewa na kampuni ya usambazaji
wa mashine hiyo ya Mindray iliyopo
nchini China.
Mafunzo hayo yalifanyika jana katika ukumbi wa JKCI ambapo
madaktari hao wamefundishwa njia maalum ya kuwachunguza wagonjwa ambao mioyo
yao imeshindwa kufanya kazi vizuri kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo
mishipa ya damu ya moyo kuziba.
Akizungumzia mafunzo hayo Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo na
Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete Dkt. Peter Kisenge alisema wataalam hao wamefundishwa njia mpya
ambayo sasa hivi inatumika duniani kote kujua uwezo wa utendaji kazi wa moyo
kwa kutumia njia iitwayo kitaalam “Sparkle tracking”.
“Mafunzo tuliyoyapa leo yametolewa na daktari bingwa kutoka
Misri ambaye amewasilisha mafunzo yake kupitia njia ya mtandao ya zoom pamoja
na daktari bingwa kutoka nchini Ethiopia ambaye alitumia mashine ya Echocardiogram
kutufundisha kwa vitendo”,
“Kupitia mafunzo haya madaktari wetu wataweza kuwasaidia
wananchi wenye uhitaji wa kufanyiwa uchunguzi kwa wagonjwa ambao mioyo yao
imeshindwa kufanya kazi na hii ni njia ambayo serikali ya awamu ya sita inatumia
kuongeza ujuzi mkubwa kwa madaktari wake ili wananchi waweze kufaidika”, alisema
Dkt. Kisenge.
Aidha Dkt Kisenge aliwaomba madaktari nchini kujitokeza pale
wanaposikia kuna mafunzo ya kibobezi yanapotolewa ili kurahisisha utendaji wao
wa kazi lakini pia kuweza kuendana na kasi ya teknolojia kwa kupata mbinu mpya
za kitabibu kama ambavyo wataalam walioshiriki mafunzo hayo wamepata na kuweza kujua
utendaji kazi wa moyo kwa kutumia njia ya “Sparkle tracking”.
“Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutuwezesha kununua
mashine hizi zenye uwezo wa hali ya juu
tunazozitumia kuwatibu wagonjwa, matarajio yetu ni kufikisha ujuzi tulioupata
hapa leo kwa wataalam wengine wa afya waliopo katika hospitali zetu za mikoa,
na wilaya”, alisema Dkt. Kisenge.
Kwa upande wake Meneja
mfumo wa picha za matibabu kutoka kampuni ya usambazaji wa mashine za Echocardiogram
ya Mindray iliyopo nchini China Li Li aliipongeza
JKCI kwa kuona umuhimu wa kuandaa mafunzo hayo ambayo yatawafanya madaktari
wanaowafanyia upimaji wa kuchunguza jinsi moyo unavyofanya kazi
(Echocardiography - ECHO) kwa wagonjwa kuendana na kasi ya maendeleo ya dunia.
“Kampuni
ya Mindray inayotengeneza mashine za ECHO ina jukumu la kutoa mafunzo pia kwa wadau wake
kama tulivyofanya hapa leo ili wadau hawa waweze kuzitumia mashine hizi kwa
ufanisi na kupata majibu sahihi ya mgonjwa kwa kumchukuza kila kitu katika moyo
wake”,.
“Hii
ni mara yetu ya kwanza kuja hapa JKCI kwa ajili ya kutoa mafunzo haya,
tunaahidi kuendelea kutoa mafunzo kama haya mara kwa mara kwa kuwaleta
madaktari mabingwa tunaofanya nao kazi kutoka pande mbalimbali za dunia ili
waweze kubadilishana uzoefu”, alisema Li.
Naye fundi sanifu wa moyo (Cardiovascular technologist) kutoka
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Paschal
Kondi alisema mafunzo yaliyotolewa na kampuni ya usambazaji wa mashine za ECHO
ya Mindray yamekuwa na faida kubwa kwake kwani ameweza kujifunza njia
mbalimbali ya upimaji wa moyo kwa kutumia mashine hiyo hivyo kuongeza ujuzi
utakaomsaidia katika utendaji kazi wake wa kazi za kila siku.
“Naushukuru uongozi wa JKCI pamoja na Kitengo cha Mafunzo na Utafiti
cha JKCI kwa kuweza kutuandalia mafunzo haya ambayo yatanifanya nifanye kazi
zangu kwa ufanisi zaidi na kuwasaidia wagonjwa ambao wanahitaji huduma hii ya
uchunguzi wa moyo kupitia mashine ya Echocardiogram”, alisema Kondi.
Comments
Post a Comment