Wauguzi JKCI washiriki bonanza la kuadhimisha siku ya wauguzi
Maafisa
Wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakivuta kamba wakati wa mashindano
ya mchezo huo kati yao na wauguzi wa Hospitali ya Mloganzila uliofanyika leo
katika viwanja vya Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam ambapo wauguzi
wa JKCI walishika nafasi ya pili. Mshindano hayo yalihusisha wauguzi kutoka
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga na
Mloganzila na Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI).
Timu ya mpira wa miguu ya maafisa wauguzi wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo
baina yao na wauguzi kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) Katika mchezo huo timu
ya JKCI ilifungwa mabao matatu na timu ya wauguzi kutoka MOI
Afisa
Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Lugendo akiwachachafya
wachezaji wa timu ya mpira wa pete ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) wakati wa
mashindano ya mchezo huo yaliyofanyika leo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha
Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam ambapo timu ya JKCI ilifungwa mabao Kumi
kwa tisa na timu hiyo.
***********************************************************
Comments
Post a Comment