Posts

Showing posts from June, 2022

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete inafanya upimaji wa magonjwa ya moyo na kisukari katika maonesho ya sabasaba

Image
  Mkurugenzi wa Kurugenzi  ya Magonjwa ya Moyo na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane akimpa kitabu cha jinsi ya kuepukana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza  mwananchi aliyetembelea banda la taasisi hiyo mwaka jana  kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo wakati wa maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yaliyofanyika  Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa. ********************************************************************************************************************************************** *********************************************************************************************************************************************   Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuwajulisha wananchi kuwa inashiriki maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika katika Uwanja wa Maonyesho wa Biashara wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ul

Wataalamu 20 kutoka Taasisi ya Moyo Uganda wajifunza utoaji wa huduma za matibabu ya moyo nchini

Image
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akiwaonesha maeneo ya Taasisi hiyo wageni kutoka Taasisi ya Moyo Uganda walipotembelea JKCI leo kwaajili ya kuangalia huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo pamoja na kujifunza namna ambavyo Taasisi hiyo inaendesha shughuli zake. Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Mkuu wa idara ya magonjwa ya moyo kwa watoto Sulende Kubhoja akielezea huduma zinazotolewa katika idara hiyo  kwa wageni kutoka Taasisi ya Moyo Uganda walipotembelea JKCI leo kwaajili ya kuangalia huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo pamoja na kujifunza namna ambavyo Taasisi hiyo inaendesha shughuli zake. Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JCKI) ambaye pia ni mkuu wa idara ya magonjwa ya moyo kwa watu wazima George Longopa akielezea huduma zinazotolewa kwa wagonjwa wa moyo wanaoudhuria kliniki katika Taasisi hiyo kwa wageni kutoka Ta

Viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete waadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa kuwatembelea wafanyakazi na wagonjwa wanaotibiwa JKCI

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi hiyo alipowatembelea katika ofisi yao kwa ajili ya kusikiliza changamoto wanazopitia katika maeneo yao ya kazi wakati wa kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akikagua taarifa za mgonjwa anayetibiwa katika Taasisi hiyo wakati wa kuhitimisha maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Utawala na Rasilimali watu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Ghati Chacha akimsikiliza mama ambaye mtoto wake amelazwa katika wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo Fatuma Mohamed alipotembelea wodi hiyo kwa ajili ya kusikiliza changamoto zinazowakabili wakati wa kuhitimisha maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Idara ya Rasilimali watu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Abdulrahman Muya a

Jukwaa la Mshua Masta latoa ngao ya ushindi kwenye sekta ya afya kwa Pro...

Image

Sensa ya watu na makazi 2022, Jitokeze kuhesabiwa

Image

Afisa muuguzi mstaafu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akabidhiwa zawadi ya hundi ya shilingi milioni tisa, cheti na ngao kutokana na utumishi wake uliotukuka

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti cha kumpongeza kwa utumishi uliotukuka Afisa Uuguzi wa JKCI Husna Mzunga ambaye amestaafu leo kwa mujibu wa sheria za   utumishi wa umma wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika   katika ukumbi wa taasisi hiyo uliopo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi ngao Afisa Uuguzi Husna Mzunga ambaye amestaafu leo kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma na kuagwa na watumishi wa Taasisi hiyo leo katika ukumbi wa JKCI uliopo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Kurugenzi ya Uuguzi Taasisi hiyo Robert Mallya. Afisa Uuguzi ambaye amestaafu leo kwa mujibu wa sheria za utumishi wa  umma Husna Mzunga akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Tshs. 9,000,000/= kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi ikiwa ni ishara ya  kumpongeza kwa utumishi wake uliotukuka wakati

RC MAKALA: Kampeni ya kupima afya bure imekuwa na mafanikio makubwa

Image
-           Awataka wananchi kuanza matibabu kwa wale waliogundulika na magonjwa yasiyoambukiza -          Awashukuru Clouds Media Group, Madaktari na wadau wengine waliofanikisha kampeni ya Afya Check -          Aelekeza uwepo wa Hospitali tembezi kwa madaktari bingwa katika kila Wilaya. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo Juni 13 amehitimisha zoezi la siku kumi za upimaji Afya bure ambapo mpaka kufikia siku ya jana Juni 12 zaidi ya wananchi 7,030 walihudumiwa na madaktari bingwa na wabobezi kutoka Hospitali kubwa za Mkoa huo. Akihitimisha zoezi hilo RC Makalla amesema zoezi hilo limekuwa na mafanikio makubwa ambapo kati ya wananchi 7,030 waliohudumiwa wananchi 1,522 walipima Shinikizo la damu, 247 Kisukari, 808 walipimwa tatizo la moyo, uchangiaji wa damu unit 203, kipimo cha ultrasound 1,726, 189 tezi dume,949 walipata chanjo ya Uviko – 19, 601 walipima Saratani ya shingo ya kizazi, 1,369 walipima tatizo la meno na macho wananchi 1,673. Kutokana na mwamko k

Wananchi Mkoa wa Dar es Salaam kupata huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo bila malipo katika kampeni ya Afya Check

Image
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tulizo Shem akimpima shinikizo la damu Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Amos Makalla ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kampeni ya upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza (Afya Check) kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam ilioandaliwa na Kampuni Clouds Media Group kwa kushirikiana na Hospitali zinazotoa huduma ya magonjwa yasiyoambukiza leo katika Viwanja vya Tanganyika Packers.  Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tulizo Shem akimpima urefu na uzito Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Amos Makalla wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza (Afya Check) kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam ulioandaliwa na Kampuni Clouds Media Group kwa kushirikiana na Hospitali zinazotoa huduma ya magonjwa yasiyoambukiza leo katika Viwanja vya Tanganyika Packers. Upimaji huo unatarajiwa kufanyika katika Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam kwa siku kumi Mkurugenz

Wananchi 437 wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo ambapo asilimia 6...

Image

Daktari bingwa wa moyo aonya madhara yatokanayo na kuacha kutumia dawa z...

Image