Afisa muuguzi mstaafu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akabidhiwa zawadi ya hundi ya shilingi milioni tisa, cheti na ngao kutokana na utumishi wake uliotukuka


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti cha kumpongeza kwa utumishi uliotukuka Afisa Uuguzi wa JKCI Husna Mzunga ambaye amestaafu leo kwa mujibu wa sheria za  utumishi wa umma wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika  katika ukumbi wa taasisi hiyo uliopo jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi ngao Afisa Uuguzi Husna Mzunga ambaye amestaafu leo kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma na kuagwa na watumishi wa Taasisi hiyo leo katika ukumbi wa JKCI uliopo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Kurugenzi ya Uuguzi Taasisi hiyo Robert Mallya.

Afisa Uuguzi ambaye amestaafu leo kwa mujibu wa sheria za utumishi wa  umma Husna Mzunga akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Tshs. 9,000,000/= kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi ikiwa ni ishara ya  kumpongeza kwa utumishi wake uliotukuka wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Winnie Masakuya akimlisha keki Afisa Uuguzi mstaafu kutoka JKCI Husna Mzunga wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Afisa Uuguzi ambaye amestaafu leo kwa mujibu wa sheria za  utumishi wa umma Husna Mzunga akimlisha keki Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini  Dar es Salaam.

     
Baadhi ya Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatili yaliyokuwa yakiendelea wakati wa hafla fupi ya kumuaga Afisa Uuguzi wa Taasisi hiyo aliyestaafu Utumishi wake wa Umma kwa mujibu wa sheria Husna Mzunga (hayupo pichani)  katika Ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo leo jijiini Dar es Salaam.

Afisa Uuguzi ambaye amestaafu leo katika Utumishi wa Umma Husna Mzunga akiwa katika picha ya pamoja na wauguzi wenzake mara baada ya kumalizika kwa  hafla fupi ya kumpongeza iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutani wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo jijini Dar es Salaam.


Picha na: JKCI

********************************************************************************************


 

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari