Viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete waadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa kuwatembelea wafanyakazi na wagonjwa wanaotibiwa JKCI


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi hiyo alipowatembelea katika ofisi yao kwa ajili ya kusikiliza changamoto wanazopitia katika maeneo yao ya kazi wakati wa kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akikagua taarifa za mgonjwa anayetibiwa katika Taasisi hiyo wakati wa kuhitimisha maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Utawala na Rasilimali watu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Ghati Chacha akimsikiliza mama ambaye mtoto wake amelazwa katika wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo Fatuma Mohamed alipotembelea wodi hiyo kwa ajili ya kusikiliza changamoto zinazowakabili wakati wa kuhitimisha maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Idara ya Rasilimali watu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Abdulrahman Muya akizungumza na wagonjwa wanaosubiria kufanyiwa kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiograph) wakati wa kuhitimisha maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa Idara ya Utawala wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Joachim Asenga akisikiliza hoja mbalimbali zilizokua zikitolewa na wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakati wa kuhitimisha maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam

 
Afisa Utawala wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Adila Lugamara akizungumza na mama wa mtoto aliyelazwa katika wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo Monica Hussen wakati wa kuhitimisha wiki ya Utumishi wa Umma leo katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam


Mkuu wa Idara ya Utawala wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Joachim Asenga akimsikiliza mzazi wa mtoto aliyelazwa katika wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo Zubeda Dominic wakati wa kuhitimisha maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam


Watumishi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakisikiliza hoja mbalimbali kwa wagonjwa walioudhuria kliniki katika Taasisi hiyo wakati wa kuhitimisha wiki ya Utumishi wa Umma leo katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.


Picha na: Genofeva Matemu

**********************************************************************************

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari