Wananchi Mkoa wa Dar es Salaam kupata huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo bila malipo katika kampeni ya Afya Check


Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tulizo Shem akimpima shinikizo la damu Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Amos Makalla ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kampeni ya upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza (Afya Check) kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam ilioandaliwa na Kampuni Clouds Media Group kwa kushirikiana na Hospitali zinazotoa huduma ya magonjwa yasiyoambukiza leo katika Viwanja vya Tanganyika Packers. 

Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tulizo Shem akimpima urefu na uzito Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Amos Makalla wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza (Afya Check) kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam ulioandaliwa na Kampuni Clouds Media Group kwa kushirikiana na Hospitali zinazotoa huduma ya magonjwa yasiyoambukiza leo katika Viwanja vya Tanganyika Packers. Upimaji huo unatarajiwa kufanyika katika Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam kwa siku kumi


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwafundisha wananchi wa Wilaya ya Kinondoni namna ya kuepuka magonjwa yasiyoambukiza ukiwemo ugonjwa wa moyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza (Afya Check) kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam ulioandaliwa na Kampuni Clouds Media Group kwa kushirikiana na Hospitali zinazotoa huduma ya magonjwa yasiyoambukiza leo katika Viwanja vya Tanganyika Packers.

Wananchi wa Wilaya ya Kinondoni wakifuatilia elimu iliyokua ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Janabi (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza (Afya Check) kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam ulioandaliwa na Kampuni Clouds Media Group kwa kushirikiana na Hospitali zinazotoa huduma ya magonjwa yasiyoambukiza leo katika Viwanja vya Tanganyika Packers. Upimaji huo unatarajiwa kufanyika katika Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam kwa siku kumi

Fundi sanifu wa Moyo (Cardiovascular Technologist) Jusmine Keria akimsomea majibu mwananchi kutoka Wilaya ya Kinondoni baada ya kumfanyia kipimo cha kuangalia mfumo wa umeme wa moyo (Electrocardiograph – ECG) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza (Afya Check) kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam ulioandaliwa na Kampuni Clouds Media Group kwa kushirikiana na Hospitali zinazotoa huduma ya magonjwa yasiyoambukiza leo katika Viwanja vya Tanganyika Packers. Upimaji huo unatarajiwa kufanyika katika Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam kwa siku kumi

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimsikiliza mwananchi aliyefika katika banda la JKCI kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza (Afya Check) kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam ulioandaliwa na Kampuni Clouds Media Group kwa kushirikiana na Hospitali zinazotoa huduma ya magonjwa yasiyoambukiza leo katika Viwanja vya Tanganyika Packers.

Wataalam wa moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakitoa huduma kwa wananchi wa Wilaya ya Kinondoni waliofika katika banda la JKCI kwa ajili ya kuchunguza afya zao wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza (Afya Check) kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam ulioandaliwa na Kampuni Clouds Media Group kwa kushirikiana na Hospitali zinazotoa huduma ya magonjwa yasiyoambukiza leo katika Viwanja vya Tanganyika Packers. Upimaji huo unatarajiwa kufanyika katika Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam kwa siku kumi

 

Picha na: Genofeva Matemu

********************************************************************************************

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari