Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete inafanya upimaji wa magonjwa ya moyo na kisukari katika maonesho ya sabasaba

 

Mkurugenzi wa Kurugenzi  ya Magonjwa ya Moyo na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane akimpa kitabu cha jinsi ya kuepukana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza  mwananchi aliyetembelea banda la taasisi hiyo mwaka jana  kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo wakati wa maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yaliyofanyika  Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa.

*******************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************

 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuwajulisha wananchi kuwa inashiriki maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika katika Uwanja wa Maonyesho wa Biashara wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 28/06/2022 hadi tarehe 13/07/2022.

Katika maonesho haya tunafanya upimaji wa afya ya moyo kwa watoto na watu wazima. Pia tunatoa chanjo ya UVIKO-19 kama kinga ya ugonjwa huu pamoja na kufanya kipimo cha kuchunguza UVIKO -19 (rapid test) kwa wale wanaosumbuliwa na tatizo katika njia ya kupumulia.

Tuna wataalamu wa lishe ambao wanatoa elimu ya lishe bora ambayo inawapa wananchi uelewa na  kufuata mtindo bora wa maisha ambao utawasaidia kuepukana na magonjwa ya moyo na kisukari ambayo ni magonjwa yasiyoambukiza na mtu anaweza kuyaepuka kwa kufuata ushauri wa kitaalamu wa lishe.

 Kwa wale watakaokutwa na matatizo ya moyo watapatiwa matibabu hii ikiwa ni pamoja na kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi yetu.

Madaktari wetu mabingwa wa magonjwa ya moyo Peter Kisenge, Tulizo Shem, Tatizo Waane, Baraka Ndelwa na Pedro Pallangyo chini ya uongozi wa Prof. Mohamed Janabi watakuwepo katika banda letu kwaajili ya kutoa huduma kwa wananchi. Nyote mnakaribishwa.

 “Tunajali Afya ya moyo yako”.

Imetolewa na : 

Anna Nkinda

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

28/06/2022

 

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari