Wataalamu wa afya 21 kutoka nchi za Eswatini, Kenya, Malawi na Tanzania washiriki mafunzo ya kufanya kipimo cha ECHO kwa watoto

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya kufanya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) kwa watoto yaliyokuwa yakitolewa na wataalamu wa JKCI na kumalizika jana jijini Dar es Salaam. Jumla ya wataalamu wa afya 21kutoka Tanzania Bara na Visiwani, nchi za Eswatini, Kenya na Malawi wamefuzu mafunzo hayo.

Wahitimu wa mafunzo ya kufanya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) kwa watoto wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo hayo iliyofanyika jana katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo jijini Dar es Salaam. Jumla ya wataalamu wa afya 21kutoka Tanzania Bara na Visiwani, nchi za Eswatini, Kenya na Malawi wamefuzu mafunzo hayo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt Peter Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa JKCI na wahitimu wa mafunzo ya kufanya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) kwa watoto wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo hayo ililyofanyika katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Jumla ya wataalamu wa afya 21kutoka Tanzania Bara na Visiwani, nchi za Eswatini, Kenya na Malawi wamefuzu mafunzo hayo


Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Shirikishi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Naizihijwa Majani akizungumza wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya kufanya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) kwa watoto yaliyokuwa yakitolewa na wataalamu wa JKCI na kumalizika jana jijini Dar es Salaam. Jumla ya wataalamu wa afya 21kutoka Tanzania Bara na Visiwani, nchi za Eswatini, Kenya na Malawi wamefuzu mafunzo hayo.


Picha Na JKCI

*************************************************************************************************************

Wataalamu wa afya 21kutoka hospitali mbalimbali Tanzania Bara na Visiwani, nchi za Eswatini, Kenya na Malawi wamefuzu mafunzo ya kufanya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) kwa watoto.

 

Mafunzo hayo ya wiki mbili ni muendelezo wa mafunzo yanayotolewa kwa wataalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) tangu mwaka 2018 kwaajili ya kuwaongezea wataalamu ujuzi katika uchunguzi wa magonjwa ya moyo kwa watoto.

 

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za Taasisi hiyo katika kuimarisha uwezo wa wataalamu na kuongeza ubora wa huduma za moyo kwa watoto nchini.

 

“Mafunzo haya ni muhimu katika kuongeza ujuzi na uwezo wa wataalamu wetu katika huduma za uchunguzi wa moyo kwa watoto ili kuhakikisha kuwa watoto wenye magonjwa ya moyo wanapata huduma bora na kwa wakati”,  alisema Dkt. Kisenge.

 

Kwa upande wake mratibu wa mafunzo hayo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  Dkt. Amanda Anyango alisema mafunzo ya kufanya kipimo cha Echocardiography kwa watoto yamekuwa na umuhimu mkubwa kwa wataalamu wanaohusika na huduma za moyo kwa watoto kwani yametoa ujuzi unaoweza kutumika katika maeneo yao ya kazi na kufanya utambuzi wa mapema kwa watoto wenye magonjwa ya moyo.

 

“Mafunzo haya yamekuwa na manufaa makubwa kwa washiriki, kwani yamewaongezea ujuzi katika kufanya uchunguzi wa moyo kwa watoto na yataende kuboresha huduma katika maeneo yao ya kazi”, alisema Dkt. Amanda.

 

Dkt. Amanda alisema mafunzo ya mara kwa mara kwa wataalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto yanaongeza ujuzi na uwezo wa kuendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia katika kuyatambua na kuyatolea ufumbuzi magonjwa ya moyo yanayowasumbua watoto.

 

Mafunzo ya kufanya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) kwa watoto ni sehemu ya jitihada za JKCI za kuendelea kuimarisha utaalamu wa ndani na wa kikanda katika kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa watoto sambamba na kuhakikisha wataalamu wanapata maarifa na ujuzi unaoendana na mahitaji ya huduma za kisasa za uchunguzi na tiba ya moyo kwa watoto.

 


Comments

Popular posts from this blog

Serikali yazindua kitabu safari ya upandikizaji wa moyo Tanzania, JKCI yaweka historia mpya ya huduma za kibobezi

Kutoka miaka 22 hadi kustaafu: Safari ya Lemmah yatoa somo kwa Watumishi wa Umma