JKCI na Mhe. Taletale kuendesha kambi ya matibabu ya moyo katika jimbo la Morogoro kusini mashariki

Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Dkt. Tulizo Shemu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo ijulikanayo kama Afya Bora na Samia itakayofanyika Mkoani Morogoro katika jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Tarafa za Ngerengere, Mikese na Mkuyuni tarehe 10 hadi 20 mwezi Novemba mwaka huu. Kambi hiyo imeandaliwa na Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Mhe. Hamisi Shaban Taletale kwa kushirikiana na JKCI.

Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Mhe. Hamisi Shaban Taletale akielezea namna ambavyo huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo zitatolewa katika jimbo la Morogoro Kusini Mashariki wakati wa uzinduzi wa kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo ijulikanayo kama Afya Bora na Samia itakayofanyika katika Tarafa za Ngerengere, Mikese na Mkuyuni tarehe 10 hadi 20 mwezi Novemba mwaka huu. Kambi hiyo imeandaliwa na Mbunge wa jimbo hilo kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Mussa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo ijulikanayo kama Afya Bora na Samia itakayofanyika Mkoani Morogoro katika jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Tarafa za Ngerengere, Mikese na Mkuyuni tarehe 10 hadi 20 mwezi Novemba mwaka huu. Kambi hiyo imeandaliwa na Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Mhe. Hamisi Shaban Taletale kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Baadhi ya viongozi kutoka Mkoa wa Morogoro na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakisikiliza wakati wa uzinduzi wa kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo ijulikanayo kama Afya Bora na Samia itakayofanyika Mkoani Morogoro katika jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Tarafa za Ngerengere, Mikese na Mkuyuni tarehe 10 hadi 20 mwezi Novemba mwaka huu. Kambi hiyo imeandaliwa na Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Mhe. Hamisi Shaban Taletale kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Na JKCI

****************************************************************************************************************************************

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Mhe. Hamisi Shaban Taletale kufanya kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo ijulikanayo kama Afya bora na Samia.

Kambi hiyo maalumu kufanyika kwa siku 10 kuanzia tarehe  10 hadi 20 Novemba 2026 katika Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki katika Tarafa za Ngerengere, Mikese na Mkuyuni ambapo wananchi watapimwa viashiria vya magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo, kupimwa vipimo vikubwa viwili vya kuchunguza moyo vya ECHO na ECG pamoja na kufanyiwa uchunguzi wa kinywa na meno.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Morogoro kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Mussa alisema Mkoa wa Morogoro jimbo la Kusini Mashariki limepata bahati ya kufikiwa na huduma bingwa za uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza bila gharama.

“Mbunge wetu Mhe. Hamisi Taletale ameunga mkono jitihada za Mhe. Rais Samia kuwafikishia wananchi wa jimbo lake huduma za matibabu bila gharama, wananchi wa Tarafa za Morogoro kusini mashariki mjitokeze kwa wingi ili muweze kutatua changamoto afya mlizonazo kupitia kambi hii”, alisema Dkt. Mussa

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Mhe. Hamisi Shaban Taletale alisema ameamua kuwafikishia wananchi wa jimbo lake huduma za afya ili wale wenye changamoto na hawakuwa na uwezo wa kufuata huduma hizo mahali zilipo waweze kupata huduma hizo kwa urahisi.

Mhe. Taletale alisema kambi hiyo ya matibabu itawaunganisha watu wote bila kuweka mipaka ya wenye nacho na wasiokuwa nacho hivyo watu wote wajitokeze kwani afya bora ujenga msingi mzuri wa uchumi wa nchi.

Aidha Mhe. Taletale alisema kupitia kambi hiyo kaya maskini 150 kutoka katika Tarafa za Ngerengere, Mikese na Mkuyuni zitakatiwa bima ya afya kupitia mpango wa bima ya afya kwa wote zilizogharamiwa na ofisi yake ikiwa ni sehemu ya kushiriki katika mikakati ya Serikali ya kuziwezesha kaya masikini kupata bima ya afya.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Dkt. Talizo Shemu alisema kupitia kambi hiyo huduma za kibingwa na ubingwa bobezi za matibabu ya moyo zitasogezwa karibu na wananchi hivyo kuongeza upatikanaji wa huduma hizo, kubaini mapema magonjwa ya moyo na vihatarishi vyake pamoja na kupunguza madhara na vifo vinavyotokana na magonjwa hayo.

“Malengo mengine ya kambi hii ni kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu magonjwa yasiyoambukiza, umuhimu wa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara, kuhamasisha jamii kuzingatia mtindo bora wa maisha na lishe bora, pamoja na kuwabaini wagonjwa wanaohitaji matibabu zaidi na kuwaunganisha na huduma za kibingwa na bobezi zinazotolewa na JKCI”, alisema Dkt. Shemu

Dkt. Shemu alisema kambi hiyo ni fursa kwa wananchi kupata huduma za uchunguzi wa afya hata kama hawana dalili zozote za ugonjwa kwani magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo yanaweza kuendelea mwilini bila kuonesha dalili katika hatua za awali na mtu anaweza kugundua tatizo wakati tayari limefikia hatua inayohitaji matibabu makubwa.

JKCI imeendeleza juhudi za kusogeza huduma za kibingwa za matibabu ya moyo karibu na wananchi kupitia kambi maalumu zinazofanyika katika maeneo mbalimbali nchini. Hadi sasa JKCI imefanikiwa kuendesha kambi za uchunguzi na matibabu ya moyo katika mikoa zaidi ya 20, ambapo jumla ya wananchi 48,354 wamefanyiwa uchunguzi wa afya.

 

Comments

Popular posts from this blog

Serikali yazindua kitabu safari ya upandikizaji wa moyo Tanzania, JKCI yaweka historia mpya ya huduma za kibobezi

Kutoka miaka 22 hadi kustaafu: Safari ya Lemmah yatoa somo kwa Watumishi wa Umma