319 wachunguzwa moyo Dodoma Festival
Afisa muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Lilian Peter akimsikiliza mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupata huduma za upimaji na matibabu ya moyo zilizokuwa zinazotolewa na wataalamu wa JKCI katika tamasha la Karibu Dodoma festival lililofanyika katika viwaja vya Chinangali park jijini Dodoma wakati akimpima kiwango cha sukari mwilini. Mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa sekya ya Afya mara baada ya kumalizika kwa tamasha la Karibu Dodoma festival lililofanyika katika viwanja vya Chinangali park. Tamasha hilo lilienda sambamba na zoezi la upimaji wa afya. Mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri akimkabidhi Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda cheti cha ushiriki wa tamasha la Karibu Dodoma festival lililomalizika jana katika viwanja vya Chinangali park. Mhasibu wa Taasisi ya Moyo Ja...