Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) waongezewa ujuzi wa jinsi ya kutumia mashine ya kuusaidia moyo kufanya kazi kwa kiwango cha juu (Intra-aortic balloon pump) na wakufunzi kutoka nchini Afrika ya Kusini
Mkufunzi wa kutumia mashine ya kuusaidia moyo
kufanya kazi kwa kiwango cha juu (Intra-aortic balloon pump) kutoka nchini Afrika
Kusini Linda Veale akiwafundisha wataalam wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) (hawapo pichani) namna ambavyo mashine hiyo inavyoweza kufanya kazi wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika leo katika
ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.
Wataalam wa afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) wakijifunza kwa vitendo namna ya kuunganisha vifaa vya
kumuunganisha mgonjwa na mashine ya kuusaidia moyo kufanya kazi kwa kiwango cha
juu (Intra-aortic balloon pump) wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika leo katika
ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi wa kutumia mashine ya kuusaidia moyo
kufanya kazi kwa kiwango cha juu (Intra-aortic balloon pump) kutoka nchini Afrika
Kusini Linda Veale akiwaonesha wataalam wa afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) namna ambavyo mashine hiyo inavyofanya kazi wakati wa mafunzo
hayo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Comments
Post a Comment