Wachezaji wawili wa klabu ya Yanga wafanyiwa vipimo vya moyo kabla ya kupatiwa leseni ya kujiunga na timu hiyo
Radiografa wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Indrisa Juma akimpima X-ray ya kifua ili kuchunguza moyo na mapafu mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Yanga Salum Salum (Sureboy) wakati wachezaji wawili wa timu hiyo walipofika katika Taasisi hiyo jana kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya ya moyo kabla ya kupata leseni ya kujiunga na timu hiyo
Daktari wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dickson Minja akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiograph - ECHO) mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Yanga Salum Salum (Sureboy) wakati wachezaji wawili wa timu hiyo walipofika katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya ya moyo kabla ya kupata leseni ya kujiunga na timu hiyo
Picha
na: JKCI
Comments
Post a Comment