Mkutano wa CardioTan 2026 wahitimishwa, wataalamu wapata ujuzi uchunguzi vipimo vya moyo
Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni Mhe. Saad Mtambule akimpatia tuzo mshindi wa kesi bora
iliyowasilishwa wakati wa mkutano wa nne wa Kimataifa wa magonjwa ya moyo –
CardioTan Imaging 2026 Dkt. Abdi Dibaba kutoka Hospitali ya Saifee wakati wa
hafla fupi ya kufunga mkutano huo iliyofanyika jana katika ukumbi wa Blue
Sapphire jijini Dar es Salaam. Jumla ya washiriki zaidi ya 600 kutoka nchi
zaidi ya 16 wameshiriki mkutano huo.
Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni Mhe. Saad Mtambule akizungumza na wataalamu wa afya walioshiriki
mkutano wa nne wa Kimataifa wa Magonjwa ya Moyo – CardioTan Imaging 2026 wakati
wa hafla fupi ya kufanga mkutano huo iliyofanyika jana katika ukumbi wa Blue
Sapphire jijini Dar es Salaam. Jumla ya washiriki zaidi ya 600 kutoka nchi zaidi
ya 16 wameshiriki mkutano huo
Mkurugenzi wa Idara ya
Upasuaji wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela
Muhozya akizungumza na washiriki wa mkutano wa nne wa kimataifa wa magonjwa ya
moyo – CardioTan Imaging 2026 kwa niaba ya mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo
Dkt. Peter Kisenge wakati wa hafla fupi ya kufunga mkutano huo iliyofanyika
jana katika ukumbi wa Blue Sapphire jijini Dar es Salaam. Jumla ya washiriki
zaidi ya 600 kutoka nchi zaidi ya 16 wameshiriki mkutano huo
Baadhi ya wataalamu wa
afya kutoka nchi mbalimbali wakifutilia mada zilizokuwa zikiendelea wakati wa
hafla fupi ya kufunga mkutano wa nne wa Kimataifa wa Magonjwa ya Moyo –
CardioTan Imaging 2026 iliyofanyika jana katika ukumbi wa Blue Sapphire jijini
Dar es Salaam. Jumla ya washiriki zaidi ya 600 kutoka nchi zaidi ya 16
wameshiriki mkutano huo.
Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni Mhe. Saad Mtambule akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
wataalamu wa afya kutoka nchi mbalimbali waliotoa mada wakati wa Mkutano wa nne
wa Kimataifa wa Magonjwa ya Moyo – CardioTan Imaging 2026 uliomalizika jana
jijini Dar es Salaam. Jumla ya washiriki zaidi ya 600 kutoka nchi zaidi ya 16
wameshiriki mkutano huo.
Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni Mhe. Saad Mtambule akichangia fedha kwaajili ya matibabu ya watoto
wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
alipotembelea banda la Taasisi isiyo ya kiserikali Heart Team Africa Foundation
(HTAF) wakati wa Mkutano wa nne wa Kimataifa wa Magonjwa ya Moyo – CardioTan
Imaging 2026 uliomalizika jana jijini Dar es Salaam. Jumla ya washiriki zaidi
ya 600 kutoka nchi zaidi ya 16 wameshiriki mkutano huo.
Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni Mhe. Saad Mtambule akiwapatia cheti cha udhamini na ushiriki wa
mkutano wa nne wa Kimataifa wa Magonjwa ya Moyo – CardioTan Imaging 2026
kampuni ya Encore Medics wakati wa hafla fupi ya kufunga mkutano huo
iliyofanyika jana katika ukumbi wa Blue Sapphire jijini Dar es Salaam. Jumla ya
washiriki zaidi ya 600 kutoka nchi zaidi ya 16 wameshiriki mkutano huo.
Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni Mhe. Saad Mtambule akiwapatia cheti cha udhamini na ushiriki wa
mkutano wa nne wa Kimataifa wa Magonjwa ya Moyo – CardioTan Imaging 2026
kampuni ya Computech Healthcare Solution wakati wa hafla fupi ya kufunga
mkutano huo iliyofanyika jana katika ukumbi wa Blue Sapphire jijini Dar es
Salaam. Jumla ya washiriki zaidi ya 600 kutoka nchi zaidi ya 16 wameshiriki
mkutano huo.
Na: JKCI
***************************************************************************************************
Mkutano wa nne wa
kimataifa wa magonjwa ya moyo – CardioTan Imaging 2026 wafungua njia kwa
wataalamu wa afya kuhakikisha magonjwa ya moyo yanaendelea kupatiwa ufumbuzi na
kuongeza ujuzi wa wanataaluma wa vipimo vya moyo kwa kutumia kipimo cha
Echocardiography.
Akizungumza wakati wa
hafla ya kufunga mkutano huo jana jijini Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni Mhe. Saad Mtambule alisema kupitia mkutano huu wataalamu wameweza
kujadili visababishi vya magonjwa ya moyo, mikakati na namna ya kujipanga ili waweze
kuongeza juhudi katika tafiti za magonjwa hayo na kuimarisha huduma zaidi.
“Tunafahamu wote kuwa
magonjwa ya moyo yamekuwa na madhara mengi ikiwemo kupata matibabu kwa muda
mrefu hivyo kuleta gharama kubwa, lakini pia husababisha vifo vingi katika
jamii zetu”, alisema Mhe. Mtambale
Mhe. Mtambale alisema Serikali
ya awamu ya sita imeendelea kuwa na maono mazuri kwa kuwekeza katika sekta ya
afya hasa upande wa magonjwa yanayohitaji utaalamu wa kibingwa.
“Kutanuka kwa huduma za
uchunguzi na matibabu ya moyo kunasaidia watu wengi kupata huduma hizo kwa urahisi
katika maeneo yao, tunaishukuru JKCI kwa utayari wa wataalamu, juhudi na moyo
mkubwa wa kiuzalendo katika kuwatibu watanzania na kuongeza ufahamu wa magonjwa
hayo katika jamii”, alisema Mhe. Mtambale
Mhe. Mtambale alisema tatizo
kubwa lililopo Tanzania kwa sasa sio wataalamu wala vifaa tiba bali kutokana na
utafiti wa mwaka 2023 inaonesha kuwa mienendo ya maisha katika jamii imekuwa ni
kichocheo kikubwa cha kupata magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo magonjwa ya moyo.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt.
Angela Muhozya akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt. Peter
Kisenge alisema mkutano huo umejikita katika upimaji wa magonjwa ya moyo
kutokana na umuhimu wa kuyatambua magonjwa hayo mapema ili matibabu yaweze kutolewa
kwa wakati na kupata matokeo mazuri.
“Tunawapongeza wataalamu
wote walioshiriki mkutano huu kwani tunaamini wamepata mambo mazuri
yatakayoweza kuwasaidia kwenda kutoa huduma bora kwa wagonjwa wa moyo”, alisema
Dkt. Angela
Dkt. Angela alisema kupitia
mkutano huo wameweza kupata vifaa vyenye intelijensia ya kisasa kuwawezesha wataalamu
waliokuja kuweze kupata elimu na kujua namna ya kuvipata na kuvitumia vifaa
hivyo.
Wakizungumza kwa
nyakati tofauti washiriki wa mkutano huo wameipongeza Serikali kupitia Wizara
ya Afya na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kuendesha mkutano huo nchini
na kuwapa ujuzi ambao utawasaidia kuwatambua wagonjwa wa moyo mapema.
Mganga Mkuu Halmashauri
ya Wilaya ya Rombo Dkt. Kandi Lusingu alisema mkutano huo ni wa muhimu kwani
umeonesha nchi ya Tanzania ilivyoendelea katika matibabu ya moyo kutokana na
uongozi mzuri wa Serikali ya awamu ya sita kuboresha huduma za afya katika
hospitali mbalimbali nchini.
“Zamani ilikuwa ni
lazima mgonjwa wa moyo kwenda nje ya nchi kupatiwa matibabu lakini kutokana na
ujuzi wa wataalamu wetu huduma hizi zinapatikana hapa nchini, pongezi nyingi
kwa JKCI kwa kuwa mstari wa mbele kutoa huduma za matibabu ya moyo, lakini pia
kutukutanisha hapa kupata utaalamu wa kuchunguza magonjwa ya moyo”, alisema
Dkt. Kandi
Dkt. Kandi alisema
kupitia mkutano huo wameweza kujifunza namna ya kufanya vipimo vya moyo kwa
wagonjwa mapema hata kwa watoto wanaozaliwa lengo likiwa ni kugundua haraka na
kutoa huduma kwa wakati.
Naye Daktari kutoka Hospitali
ya Wilaya ya Tabora Tumaini Fumbuka alisema mkutano huo umekuwa chachu kwa
watoa huduma wa hospitali za wilaya kuweza kubaini magonjwa ya moyo na
kuwaelekeza wananchi wenye magonjwa hayo kwenda sehemu sahihi kupata huduma kwa
wakati.
Dkt. Fumbuka alisema
kupitia mkutano huo wameweza kuhamasishwa kuhusu upimaji wa picha sahihi, na ubainifu
wa magonjwa ya moyo katika vituo vya afya na hospitali za wilaya kutokana na
magonjwa hayo kukua kwa kasi.
Mkutano wa nne wa
kimataifa wa magonjwa ya moyo – CardioTan Imaging 2026 wenye kauli mbiu “Uchunguzi
mahiri kwa moyo imara” umewakutanisha wataalamu wa afya zaidi ya 600 kutoka nchi
zaidi ya 16, pia kupitia mkutano huo Chama cha wataalamu wa kupima moyo kwa
kutumia kipimo cha Echocardiography Tanzania (Echocardiograph society)
kilizinduliwa.



Comments
Post a Comment