Posts
Showing posts from 2020
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) yaombwa kufikisha uelewa wa magonjwa ya moyo mashuleni
- Get link
- X
- Other Apps
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Winnie Masakuya akitoa uelewa wa jinsi ya kutunza moyo ili uwe na afya njema kwa walimu wakuu wa shule za Sekondari nchini waliofika katika banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupima viashiria vya magojwa ya moyo wakati wa mkutano wa walimu hao unaomalizika hivi karibuni jijini Dodoma. Walimu wakuu wa shule za Sekondari nchini wameiomba Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kuhakikisha uelewa wa magonjwa ya moyo unatolewa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na siyo kwa watu wazima peke yao. Wamesema uelewa wa magonjwa hayo ukiwafikia wanafunzi utawasaidia kuitunza mioyo yao na hivyo kuweza kuishi maisha marefu zaidi tofauti na inavyofanyika kwa sasa ambapo uelewa unatolewa kwa watu wazima wengi wao wakiwa na umri wa kuanzia miaka 35 na kuendelea. Ombi hilo limetolewa hivi karibuni na baadhi ya walimu waliohudhuria mkutano wa 15 wa walimu wakuu wa shule za sekondari nchini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano...
Prof. Janabi awafundisha walimu wakuu wa shule za sekondari namna ya kue...
- Get link
- X
- Other Apps
Walimu nchini wapewa mbinu zitakazowawezesha kufaidi matunda ya uchumi wa kati katika miaka ijayo
- Get link
- X
- Other Apps

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akitoa mada kuhusu magonjwa ya moyo na jinsi ya kuyaepuka kwa walimu waliohudhuria mkutano wa walimu wakuu wa shule za sekondari nchini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete uliopo jijini Dodoma. JKCI imeshiriki katika mkutano huo kwa kufanya upimaji wa viashiria vya magonjwa ya moyo pamoja na kutoa uelewa (awareness) wa magojwa hayo. Na Veronica Mrema – Dodoma Walimu nchini wamepewa mbinu zitakazowawezesha kufaidi matunda ya uchumi wa kati katika miaka ijayo, miongoni mwa mambo muhimu waliyohimizwa kuyazingatia ni kutunza afya zao. Wamehimizwa pia kuepuka uzito uliokithiri na kufanya mara kwa mara uchunguzi wa afya ili kujua hali zao na kutibiwa mapema ikiwa watagundulika tayari wameanza kushambuliwa na magonjwa mbalimbali hususan yasiyoambukiza ambayo hivi sasa ni janga la dunia. Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa. Moh...
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) yafanya upimaji wa viashiria vya magonjwa ya moyo pamoja na kutoa uelewa wa magojwa hayo katika mkutano wa walimu wakuu wa shule za sekondari nchini unaofanyika jijini Dodoma
- Get link
- X
- Other Apps

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akitoa mada kuhusu magonjwa ya moyo na jinsi ya kuyaepuka kwa walimu waliohudhuria mkutano wa walimu wakuu wa shule za sekondari nchini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete uliopo jijini Dodoma. JKCI imeshiriki katika mkutano huo kwa kufanya upimaji wa viashiria vya magonjwa ya moyo pamoja na kutoa uelewa (awareness) wa magojwa hayo. Baadhi ya walimu wakuu wa shule za Sekondari nchini wakimsikiliza Prof. Mohamed Janabi wakati akitoa mada kuhusu magojwa ya moyo na jinsi ya kuyaepuka wakati wa mkutano mkuu wa walimu hao uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete uliopo jijini Dodoma. JKCI imeshiriki katika mkutano huo kwa kufanya upimaji wa viashiria vya magonjwa ya moyo pamoja na kutoa uelewa (awareness) wa magojwa hayo. Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwapima walimu wakuu wa shule za Sekondari nchini viashiria vya mag...
Heart diseases services at Jakaya Kikwete Cardiac Institute, Tanzania
- Get link
- X
- Other Apps
Wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) waonesha huduma wanazozitoa kwa wagonjwa wanaowahudumia katika taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi wa mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee .
- Get link
- X
- Other Apps

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Agnes Lugendo akimweleza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Aboubakar Kunenge jinsi wauguzi wa Taasisi hiyo wanavyohudumia wagonjwa waliolazwa wodini wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi wa Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Karimejee. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amewapongeza Wauguzi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya ya kuokoa maisha ya wagonjwa jambo lililosaidia kupunguza vifo. Rc Kunenge alisema hayo hivi karibuni wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi wa Mkoa wa Dar es salaam yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee na kuwahimiza kuendelea kuchapa kazi kwa uwezo wao wote na kuwaahidi kwamba Serikali itaendelea kushirikiana nao bega kwa bega. Aidha RC Kunenge alisema anafurahi kuona hata zile kelele za wananchi kuhusu lugha chafu zimepungua na badala yake hivi sasa wauguzi wamekuwa na lugha ya upendo kwa wagonjwa jambo linalotia faraja...
Daktari wa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Parvina Kazahura awa mshindi wa kwanza wa kundi la tafiti za kuzuia magojwa yasiyo ya kuambukiza
- Get link
- X
- Other Apps

Katibu Mkuu wizara ya Afya Prof. Mabula Mchembe akimkabidhi Daktari wa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Parvina Kazahura cheti cha mshindi wa kwanza wa kundi la tafiti za kuzuia magojwa yasiyo ya kuambukiza ambaye alifanya utafiti wa kugundua mapema magonjwa ya valvu za moyo kwa watoto wa shule za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam . Dkt. Parvina alikabidhiwa cheti hicho hivi karibuni wakati wa kongamano la pili la kitaifa la sayansi la magonjwa yasiyoambukiza lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wizara ya Afya Prof. Mabula Mchembe akimkabidhi Daktari wa Chuo Kikuu cha Dodoma Azan Nyundo cheti cha mshindi wa kwanza wa utafiti alioufanya kuhusu tabia hatarishi za magonnjwa ya moyo kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Mirembe wanaotumia dawa za magonjwa ya akili wakati wa kongamano la pili la kitaifa la sayansi la magonjwa yasiyoambukiza lililomalizika ...
Kampuni ya Vunja bei yatoa zawadi za vyombo kwa wafayakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
- Get link
- X
- Other Apps

Mkurugenzi wa Kampuni ya Vunja bei Shija Kamanija akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) mara baada ya kufika katika taasisi hiyo kwa ajili ya kuwapa zawadi za vyombo na kuwauzia bidhaa hizo kwa bei naafuu. Kampuni hiyo ilifanya hivyo ikiwa ni moja ya njia ya kufikisha huduma wanayoitoa kiurahisi kwa wafanyakazi hao pamoja na kuwapa motisha ya kazi wanayoifanya ya kutibu wagonjwa wenye matatizo ya moyo. Mkurugenzi wa Kampuni ya Vunja bei Shija Kamanija akimpa zawadi ya boxi lenye glasi za kuywea juice Dominick Kanani ambaye ni mfanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) mara baada ya kufika katika taasisi hiyo kwa ajili ya kutoa zawadi za vyombo na kuwauzia wafanyakazi bidhaa hizo kwa bei naafuu. Kampuni hiyo ilifanya hivyo ikiwa ni moja ya njia ya kufikisha huduma wanayoitoa kiurahisi kwa wafanyakazi hao pamoja na kuwapa motisha ya kazi wanayoifanya ya kutibu wagonjwa wenye matatizo ya moyo. ...
Wafanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete wapongezwa kwa utendaji mzuri wa kazi
- Get link
- X
- Other Apps

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Utawala na Fedha wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA Agnes Kuhenga akisoma majina ya wafanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 wa Taasisi hiyo ambapo wafanyakazi watatu walichaguliwa na kupewa zawadi mbalimbali za kuwapongeza kutokana na utendaji wao mzuri wa kazi. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi zawadi ya ngao mfanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 aliyeshika nafasi ya kwanza George Msabila wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora watatu iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Mfanyakazi huyo pia alipewa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni moja na laki tano. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi zawadi ya cheti mfanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 aliyeshika nafasi ya pili Dkt. Henry Mayala wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyaka...
Wanawake ‘watoa ya moyoni’ Jukwaa la Women Health Talk
- Get link
- X
- Other Apps

Miss Tanzania 2001 Happiness Magese akiuliza swali wakati wa Jukwaa la Women Health Talk 2020 lililofanyika Jijini Dar es Salaam lililoandaliwa na Doctor's Plaza Polyclinic kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), GSM Tanzania, Hyatt Regency Hotel, MultiChoise Tanzania (DSTV), Ajanta Pharma na Masilamani KasMedics. Wanawake wanakabiliwa na changamoto nyingi ambazo hawana majibu yake, wengine hawajui wapi wanakoweza kupata ufumbuzi, hali inayowasababishia baadhi yao kujikuta wakipata magonjwa mbalimbali na hata unyanyaswaji wa kijinsi na kingono. Yamebainishwa hayo wakati wa majadiliano kwenye Jukwaa la Women Health Talk 2020 lililowakutanisha wanawake wa taaluma mbalimbali pamoja na wataalamu mabingwa wa magonjwa ya binadamu ikiwamo ya kina mama, moyo, saratani na kisukari. Akiwasilisha mada katika Jukwaa hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Tanzania Health Promotion Support (THPS), Dk. Redempta Mbatia alisema wapo baadhi ya wanawake wali...
TUGHE- JKCI yaishukuru menejimenti ya JKCI kwa uongozi sikivu
- Get link
- X
- Other Apps

Mhadhiri wa chuo kikuu cha Tumaini Dkt. Mtaki akitoa mada ya sheria za kazi kwa wajumbe wa kikao cha nne cha baraza la wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. Baraza huru na uongozi sikivu wa menejimenti ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inayoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Profesa Mohamed Janabi ni mafanikio makubwa ambayo uongozi wa Baraza la nne la Wafanyakazi wa Taasisi hiyo umejivunia hatua ambayo imetajwa kuimarisha utendaji kazi na kuboresha huduma kwa wananchi. Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo wakati wa kikao cha nne cha baraza baraza la wafayakazi kilichofanyika Protea Hotel jijini hapa, Katibu wa chama cha wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya (TUGHE) tawi la JKCI, Joyce Mugala amesema Menejimenti hiyo imekuwa ikipokea hoja zao na kuzifanyia kazi kwa wakati. “Limekuwa baraza lenye mafanikio, tumeona Mkurugenzi Mtendaji amekuwa akipokea na kufan...