Serikali yaombwa kuyaingiza magonjwa yasiyoambukiza katika bima ya afya kwa watu wote
Katibu wa Shirikisho la Vyama vya magonjwa yasiyoambukiza Tanzania (TANCDA) Prof. Kaushik Ramaiya akiwasilisha mada kuhusu ukubwa wa tatizo la magonjwa yasiyoambukiza wakati wa uzinduzi wa mkakati wa utetezi juu ya bima ya afya kwa watu wote inayojumuisha magonjwa yasiyoambukiza uliofanyika hivi karibuni katika Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo uliandaliwa na Shirikisho la Vyama vya magonjwa yasiyoambukiza Tanzania (TANCDA). Katibu wa Shirikisho la Vyama vya magonjwa yasiyoambukiza Tanzania (TANCDA) Prof. Kaushik Ramaiya akizungumza na wadau wa afya walioshiriki katika uzinduzi wa mkakati wa bima ya afya kwa wote inayojumuisha magonjwa yasiyoambukiza uliofanyika hivi karibuni katika Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam. Walioshiriki katika uzinduzi huo ni wadau mbalimbali wakiwemo wizara ya Afya, wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI, Kifua Kikuu, Dawa za kulevya na Magonjwa yasiyoambukiza, Kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya ...