Wanawake watakiwa kuandaa mlo bora ili kuzikinga familia zao na magonjwa yasiyoambukiza
Washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuyafahamu magonjwa yasiyoambukiza ambao ni wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI, Kifua kikuu, madawa za kulevya na magonjwa yasiyoambukiza, watu wanaoishi na magonjwa hayo na wahariri wa vyombo vya habari wakifuatilia mada ya umuhimu wa kufanya mazoezi iliyokuwa inatolewa kwenye mafunzo hayo yanayofanyika katika Ukumbi wa Protea jijini Dar es Salaam. Mfunzo hayo ya siku mbili yameandaliwa na Wizara ya Afya kupitia Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukiza Tanzania (TANCDA).
Mkurugenzi Msaidizi huduma za lishe kutoka Wizara ya Afya Dkt. Grace Moshi akiwasilisha mada kuhusu lishe bora inavyoweza kuwakinga watu na magonjwa yasiyoambukiza kwa washiriki wa mafunzo ya kujenga uwezo wa kuyafahamu magonjwa hayo ambao ni wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI, Kifua kikuu, madawa za kulevya na magonjwa yasiyoambukiza, watu wanaoishi na magonjwa hayo na wahariri wa vyombo vya habari . Mafunzo hayo ya siku mbili yanayofanyika katika Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam yameandaliwa na Wizara ya Afya kupitia Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukiza Tanzania (TANCDA).
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukiza Tanzania (TANCDA) Prof. Andwer Swai akitoa mada ya ugonjwa wa kisukari kwa washiriki wa mafunzo ya kuwajenga uwezo wa kuyafahamu magonjwa yasiyoambukiza ambao ni wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI, Kifua kikuu, madawa za kulevya na magonjwa yasiyoambukiza, watu wanaoishi na magonjwa hayo na wahariri wa vyombo vya habari . Mafunzo hayo ya siku mbili yanayofanyika katika Hoteli ya Protea iliyopo jijini Dar es Salaam imeandaliwa na Wizara ya Afya kupitia Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukiza Tanzania (TANCDA).
Washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa
kuyafahamu magonjwa yasiyoambukiza ambao ni wajumbe wa kamati ya kudumu ya
bunge ya masuala ya UKIMWI, Kifua kikuu, madawa za kulevya na magonjwa yasiyoambukiza,
watu wanaoishi na magonjwa hayo na wahariri wa vyombo vya habari wakifuatilia
mada ya umuhimu wa kufanya mazoezi iliyokuwa inatolewa kwenye mafunzo hayo
yanayofanyika katika Ukumbi wa Protea jijini Dar es Salaam. Mfunzo hayo ya siku mbili yameandaliwa na Wizara ya Afya
kupitia Shirikisho la Vyama vya Magonjwa
yasiyoambukiza Tanzania (TANCDA).
Washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa
kuyafahamu magonjwa yasiyoambukiza ambao
ni wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI, Kifua kikuu,
madawa za kulevya na magonjwa yasiyoambukiza, watu wanaoishi na magonjwa hayo na wahariri wa
vyombo vya habari wakiwa katika picha ya
pamoja mara baada ya kufunguliwa kwa mafunzo hayo yanayofanyika katika Hoteli
ya Protea jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo ya siku mbili yameandaliwa na
Wizara ya Afya kupitia Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukiza
Tanzania (TANCDA).
Wanawake nchini wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika
kuzikinga familia zao dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza kwa kuandaa mlo bora
kwani magonjwa hayo yanatokana na mtindo mbaya wa maisha ikiwa ni pamoja na
kula vyakula bila mpangilio.
Rai hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Malinyi
Mhe. Antipas Mgungusi katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuyafahamu magonjwa yasiyoambukiza
wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya
UKIMWI, Kifua kikuu, madawa za kulevya na magonjwa yasiyoambukiza, watu
wanaoishi na magonjwa hayo na wahariri wa vyombo vya habari yanayofanyika
katika Hoteli ya Protea iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mhe. Mgungusi alisema mkurugenzi wa masuala ya
chakula na lishe katika familia ni mwanamke na kuwataka wanawake katika familia
kuchukua majukumu yao ya kuhakikisha familia zinapata chakula bora kisichokuwa na mafuta
mengi, sukari nyingi na chumvi nyingi ili kuzikinga na magonjwa yasiyoambukiza.
“Mara nyingi sisi wanaume tukitoka katika
mihangaiko yetu tukifika nyumbani tunakula chakula tulichoandaliwa mezani,
hivyo basi kama mama kaandaa chakula hatarishi kwa afya tunakula lakini pia
kama kaandaa chakula chenye afya bora tutakula. Hivyo ni vyema wanawake kuwa mstari wa mbele katika
kuokoa familia zao na magonjwa haya yasiyoambukiza”, alisema Mhe. Mgungusi.
Mhe. Mgungusi ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya
kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI, Kifua kikuu, madawa za kulevya na
magonjwa yasiyoambukiza aliwaomba wadau wa maendeleo nchini kuungana kwa pamoja kutafuta
mbinu zitakazowezesha magonjwa yasiyoambukiza yanapungua kwani magonjwa hayo hutumia
gharama nyingi kuyatibu na kuzifanya
familia kubaki maskini.
“Changamoto ya magonjwa yasiyoambukiza ni kubwa,
tumeona watu wengi wanapoteza maisha, lakini pia magonjwa haya yanafahamika
kuwa ni magonjwa ambayo tiba zake ni za gharama kubwa. Ni vyema jamii ikatumia
njia mbalimbali za kujikinga na magonjwa haya kwani gharama za kujikinga ni
ndogo kuliko gharama za matibabu endapo mtu atapata magonjwa haya”, .
“Nikitoka hapa nitachukua jukumu langu la msingi la
kuelimisha watu juu ya magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo, kansa, kisukari, pumu na
selimundu kwani watu wengi hawana uelewa wa kutosha kuhusu magonjwa haya hivyo
kupelekea wagonjwa kugundulika kuwa na matatizo haya wakiwa katika hatua mbaya”,
alisema Mhe. Mgunguzi.
Kwa upande wake Meneja wa elimu ya afya kwa umma na
kaimu meneja kitengo cha magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar Bakari Magarawa aliipongeza Serikali kupitia Wizara ya
Afya na wadau binafsi kwa juhudi zao za kupambana na magonjwa hayo.
Magarawa aliwaomba wadau kuendelea
kuhamasisha jamii namna inavyoweza
kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza kwa kuanzisha mafunzo mbalimbali yanayotoa
elimu katika makundi rika na kuikinga jamii na magonjwa yasiyoambukiza.
“Ni jukumu letu kila mtu kwa wakati wake kupambana
na kuipambania jamii iliyotuzunguka ili kwa pamoja tuweze kutokomeza magonjwa
yasiyoambukiza ambayo yamekuwa yakitumia gharama kubwa kuyatibu hivyo kupelekea
uchumi wa nchi na uchumi wa familia kutumika katika matibabu badala ya kutumika
katika maendeleo mengine”, alisema Magarawa.
Akizungumza kuhusu mafunzo hayo Mhariri Mkuu wa
Clouds Media Group na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake
Tanzania (TAMWA) Joyce Shebe alisema mafunzo
ya kuwajengea uwezo aliyoyapata yamemfungua
macho na kuona ukubwa wa tatizo hivyo kumpa jukumu kama mwandishi wa habari kuisaidia
jamii kutoa taarifa za kuelimisha umma ili kupunguza vifo vinavyosababishwa na
magonjwa yasiyoambukiza.
Joyce alisema waandishi wa habari wanapaswa
kuisaidia jamii ya watanzania ili iweze kuepuka kupata magonjwa yasiyoambukiza
kwa kutumia vyombo vyao vya habari wataweza kuhamasisha mbinu ambazo zitazuia
magonjwa hayo kama kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi, kula vyakula bora na
kufuata mtindo bora wa maisha ili kujikinga na magonjwa hayo.
“Ninaiomba Serikali iwe inatoa takwimu za
magonjwa haya kwa kutupa nafasi ya kujua ukubwa wa tatizo ili kwa pamoja sisi
kupitia vyombo vyetu vya habari tuingie kwenye vita ya kupambana na magonjwa
haya na kuikinga jamii yetu na magonjwa yasiyoambukiza”, alisema Joyce.
Naye Mbunge wa Vitu Maalum kutoka Mkoa wa Pwani ambaye
pia mjumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI, Kifua kikuu,
madawa za kulevya na magonjwa yasiyoambukiza Mhe. Hawa Chakoma aliipongeza Serikali
kwa jitihada inayofanya ya kupambana na magonjwa
hayo kwa kutenga bajeti inayotumika
kununua vifaa tiba, dawa na kuwasaidia wagonjwa wenye magonjwa yasiyoambukiza.
“Magonjwa yasiyoambukiza yamekuwa yakichukua
bajeti kubwa ya Serikali katika kuyatibu, ni jukumu letu sasa kupaza sauti zetu
ili kuyapunguza ikiwezekana kuyaondoka kabisa magonjwa haya kwani hayahitaji
bajeti kuyaondoa bali uhitaji jitihada zetu katika kujikinga nayo”, alisema
Mhe. Hawa
Aidha Mhe. Hawa alilipongeza Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukiza Tanzania (TANCDA) kwa kuwa mstari wa mbele katika kupambana
kwa ajili ya kuikinga jamii na magonjwa hayo kwa kutoa mafunzo mbalimbali na
kuwafikia wagonjwa ambao tayari wanaishi na magonjwa hayo ili wawe ushuhuda katika jamii kwa kujitokeza na kutoa
changamoto mbalimbali wanazopitia.
Mafunzo hayo ya siku mbili yanayohudhuriwa na
washiriki 64 yameandaliwa na Wizara ya Afya kupitia Shirikisho la Vyama vya
Magonjwa yasiyoambukiza Tanzania
(TANCDA).
Comments
Post a Comment