Watu 26 kati ya 100 wana tatizo la ugonjwa wa shinikizo la juu la damu nchini
Amina Mollel mkazi wa Arusha ambaye anaishi na ugonjwa wa saratani ya kizazi na Virusi vya UKIMWI akieleza jinsi anavyoishi na magonjwa hayo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuyafahamu magonjwa yasiyoambukiza yaliyoandaliwa kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI, Kifua kikuu, madawa ya kulevya na magonjwa yasiyoambukiza, watu wanaoishi na magonjwa hayo na wahariri wa vyombo vya habari. Washiriki 64 walihudhuria mafunzo hayo ya siku mbili yaliandaliwa na Wizara ya Afya kupitia Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukiza Tanzania (TANCDA) yaliyofanyika katika Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuyafahamu magonjwa yasiyoambukiza ambao ni wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI, Kifua kikuu, madawa ya kulevya na magonjwa yasiyoambukiza, watu wanaoishi na magonjwa hayo na wahariri wa vyombo vya habari wakiwa katika makundi wakijadili sheria mbalimbali zitakazosaidia kutokomeza magonjwa hayo. Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyomalizika jana katika Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam yaliandaliwa na Wizara ya Afya kupitia Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukiza Tanzania (TANCDA).
Washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuyafahamu magonjwa yasiyoambukiza ambao ni wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI, Kifua kikuu, madawa ya kulevya na magonjwa yasiyoambukiza, watu wanaoishi na magonjwa hayo na wahariri wa vyombo vya habari wakiwa katika makundi wakijadili sheria mbalimbali zitakazosaidia kutokomeza magonjwa hayo. Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyomalizika jana katika Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam yaliandaliwa na Wizara ya Afya kupitia Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukiza Tanzania (TANCDA).
George Kwayu mkazi wa Dar es Salaam ambaye anaishi na ugonjwa wa kisukari akielezea changamoto alizokutana nazo mara baada ya kugundulika kuwa na ugonjwa huo kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuyafahamu magonjwa yasiyoambukiza yaliyoandaliwa kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI, Kifua kikuu, madawa ya kulevya na magonjwa yasiyoambukiza, watu wanaoishi na magonjwa hayo na wahariri wa vyombo vya habari. Washiriki 64 walihudhuria mafunzo hayo ya siku mbili yaliandaliwa na Wizara ya Afya kupitia Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukiza Tanzania (TANCDA) yaliyofanyika katika Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam.
Meneja Mradi kutoka Shirikisho la Vyama vya
Magonjwa yasiyoambukiza Tanzania
(TANCDA) Happy Nchimbi akieleza jinsi shirikisho hilo linavyofanya kazi
kwenye mafunzo ya kujenga uwezo wa kuyafahamu magonjwa yasiyoambukiza
iliyotolewa kwa wajumbe wa kamati ya
kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI, Kifua kikuu, madawa ya kulevya na
magonjwa yasiyoambukiza, watu wanaoishi na magonjwa hayo na wahariri wa vyombo
vya habari . Mafunzo hayo ya siku mbili
yaliyomalizika jana yaliyofanyika katika Hoteli ya Protea jijini Dar es
Salaam yaliandaliwa na Wizara ya Afya kupitia Shirikisho la Vyama vya Magonjwa
yasiyoambukiza Tanzania (TANCDA).
Picha na Henrick Chiwangu
***************************************************************************************************************
Utafiti wa viashiria vya magonjwa yasiyoambukiza
uliofanyika nchini mwaka 2012 unaonesha watu 26 kati ya 100 wanamatatizo ya
magonjwa ya shinikizo la juu la damu na tisa kati ya 100 wanamatatizo ya
kisukari.
Aidha hadi sasa kuna visa vipya vya magonjwa ya saratani
takribani elfu 40 kwa mwaka na ongezeko kubwa la magonjwa ya figo yanayohitaji
usafishwaji wa damu na upandikizwaji wa figo.
Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi Msaidizi
Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya Dkt. James Kiologwe wakati akizungumza
katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuyafahamu magonjwa yasiyoambukiza
yaliyoandaliwa kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI,
Kifua kikuu, madawa ya kulevya na magojwa yasiyoambukiza, watu wanaoishi ya
magonjwa hayo na na wahariri wa habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Protea
jijini Dar es Salaam.
Dkt. Kiologwe alisema kuongezeka kwa wagonjwa
wenye matatizo ya magonjwa
yasiyoambukiza kumeifanya Serikali kutumia fedha nyingi kuyatibu
magonjwa hayo hivyo basi ni lazima kuwepo na uwekezaji mkubwa na wakutosha ili
kuzuia watu wasipate magonjwa hayo, lakini wale wachache watakaopata magonjwa
hayo watambulike mapema kabla hawajapata
madhara zaidi na hii itasaidia kukuza uchumi wa nchi wetu kwasababu jamii yenye
afya bora hushiriki vizuri katika kukuza maendeleo ya nchi.
“Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Kassim Majaliwa alizindua programu ya taifa ya kuzuia na kudhibiti
magonjwa yasiyoambukiza mwaka 2019 ili kuongeza chachu ya kupambana na magonjwa
yasiyoambukiza nchini yanayoongezeka kwa kasi nasi tupo hapa kuendeleza
gurudumu hilo ili kujenga jamii isiyo na magonjwa yasiyoambukiza”,.
“Kampeni ya kitaifa ya kubadilisha mtindo wa
maisha italenga zaidi kutoa elimu kwasababu elimu ndio njia kubwa itakayoweza
kuokoa maisha ya jamii yetu lakini pia kupata ushiriki mpana wa sekta
mbalimbali katika kuzuia vichocheo
vinavyosababisha magonjwa yasiyoambukiza”, alisema Dkt. Kiologwe.
Aidha Dkt. Kiologwe alisema katika mafunzo hayo
wajumbe wamefanya uchambuzi wa kisera
kuhusiana na masuala ya lishe kwasababu suala la ulaji ni suala mtambuka ambalo
linahitaji ushiriki wa sekta mbalimbali kuangalia namna vyakula vinavyopatikana
na kuandaliwa kama vile vyakula vya sukari, vyakula vyenye chumvi, pombe na
vimiminika vingine vinavyozalishwa na kutumika.
“Baada ya uchambuzi huo wa kisera wadau
wanatarajia kutumia chambuzi na takwimu watakazopata kutengeneza kampeni ya
kitaifa ya kubadilisha mtindo wa maisha kwa itakayosaidia kuondoa viashiria na
changamoto mbalimbali zinazopeleka watu kupata magonjwa yasiyoambukiza”,
alisema Dkt. Kiologwe.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Kisukari
Tanzania (TDA) na mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukiza
Tanzania (TANCDA) Prof. Andrew Swai alisema wadau mbalimbali walianza kufanya
tafiti za magonjwa yasiyoambukiza ili kuona yameenea kwa kiasi gani tangu mwaka
1986 ambapo kwa wakati huo ilionekana watu kutoka maeneo ya vijijini ndio
walikuwa na magonjwa yasiyoambukiza kwa wingi.
“Mwaka 1986 tafiti zilizofanyika katika mkoa wa
Dar es Salaam zilionesha asilimia 3 ya watu walikutwa na ugonjwa wa kisukari,
asilimia 5 walikutwa na Shinikizo la damu na mafuta kuzidi kwenye damu ilikua
ni aslimia 5 lakini sasa kutokana na maendeleo na teknolojia asilimia ya
magonjwa yasiyoambukiza yanazidi kukuwa kwa kasi hasa maeneo ya mijini”,
“Magonjwa yasiyoambukiza kwa kiwango kikubwa
yamekuwa yakichochewa na vichocheo mtambuka kama vile mitindo isiyo bora ya
maisha hasa ulaji usiofaa, kutokufanya mazoezi, unywaji wa vilevi, na matumizi
ya sigara, ni wakati sasa jamii ibadilike magonjwa haya yasiwe tena vizuizi vya
maendeleo katika familia zetu”, alisema Prof. Swai.
Amina Mollel mkazi wa Arusha ambaye anaishi na saratani ya kizazi na Virusi vya UKIMWI alisema
mfumo wa maisha aliokuwa akiuishi ulipelekea yeye kupata saratani ya shingo ya
kizazi ugonjwa ambao jamii yake hawakuupokea vizuri hivyo kumfanya kuwa mnyonge
katika jamii yake lakini baada ya kuhudhuria kliniki na kupata elimu sahihi
amekuwa mtoa elimu ngazi ya jamii hivyo kufikisha elimu sahihi ya ugonjwa huo
katika jamii inayomzunguka.
“Nilivyomaliza kliniki yangu ya kwanza katika Taasisi
ya Saratani Ocean Road na kurudi mtaani
nilishangaa watu wengi ukiongelea saratani hawajui kama ndio kansa na
ukiongelea kansa hawajui kama ndio saratani hivyo kugundua kuwa elimu ya
magonjwa yasiyoambukiza bado haipo katika ngazi za jamii”,.
“Nimefurahi leo kuona katika mkutano huu
waandishi wa habari wamealikwa, wanapotoka hapa wakawe chachu ya kuilisha jamii
elimu ya magonjwa yasiyoambukiza, yanasababishwa na nini, changamoto zake na nini
kifanye ili jamii isipate magonjwa hayo kwani kwa kufanya hivyo watakuwa
wameokoa maisha ya watu wengi”, alisema Amina.
Naye George Kwayu ambaye ni mgonjwa wa kisukari
kwa miaka 23 sasa alisema wagonjwa wa kisukari wamekuwa wakipitia changamoto
mbalimbali ikiwemo upokeaji hasi wa tatizo la kisukari na jamii kuwa na mtazamo
hasi juu ya ugonjwa huo hivyo kuwakatisha tamaa wagonjwa hao.
Kwayu alisema wagonjwa wa kisukari kama watafuata
maelekezo wanayopewa na wataalam wa afya maisha yao yatarejea katika hali ya
kawaida kwani wengi hupoteza maisha kwa kudharau ama kutokufuata maelekezo
waliyopewa na wataalam wa afya na wengine hupoteza maisha kutokana na ugumu wa
maisha hivyo kushindwa kumudu gharama za matibabu.
“Nimepitia changamoto nyingi tangu nikiwa mdogo
baada ya kugundulika ninatatizo la kisukari nikiwa na umri wa miaka mitatu,
shule nyingi zilikuwa zikinikataa kuwa naweza kuanguka na kufa wakati wowote
hivyo kunipa wakati mgumu katika kutimiza ndoto zangu, lakini pia jamii imekuwa
ikitunyooshea mkono kuwa sisi wagonjwa wa kisukari hatuwezi kupata watoto
pasipo kuwa na elilmu juu ya ugonjwa huu wa kisukari”, alisema Kwayu.
Washiriki 64 walihudhuria mafunzo hayo ya siku mbili yaliandaliwa na Wizara ya Afya kupitia Shirikisho la Vyama vya Magonjwa
yasiyoambukiza Tanzania (TANCDA) yaliyofanyika katika Hoteli ya Protea jijini
Dar es Salaam.
Comments
Post a Comment