JKCI mbioni kushirikiana na Jamhuri ya watu wa Czech kutoa huduma za matibabu ya moyo

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akijadiliana na madaktari kutoka Hospitali ya Ostrava iliyopo Jamhuri ya Watu wa Czech namna ambayo watashirikiana katika kutoa huduma za matibabu ya moyo jana baada ya madaktri hao kutembelea JKCI Jijini Dar es Salaam

Madaktari kutoka Hospitali ya Ostrava iliyopo nchini Czech na wenzao kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia majadiliano wakati madaktari hao walipotembelea JKCI kwa ajili ya kuona namna ya kushirikiana katika kutoa huduma za matibabu ya moyo jana katika ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam

Afisa Muuguzi wa Chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prisca Kiyuka akiwaelezea namna ambavyo wagonjwa wanapatiwa huduma katika chumba hicho madaktari kutoka Hospitali ya Ostrava iliyopo Jamhuri ya Watu wa Czech walipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuona namna ambavyo wanaweza kushirikiana katika kutoa huduma za matibabu ya moyo jana Jijini Dar es Salaam


Fundi sanifu wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kulindwa Kasubi akiwaelezea huduma ya upasuaji mdogo wa moyo inayotolewa katika chumba cha Cath Lab madaktari kutoka Hospitali ya Ostrava iliyopo Jamhuri ya Watu wa Czech walipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuona namna ambavyo wanaweza kushirikiana katika kutoa huduma za matibabu ya moyo jana Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi katika picha ya pamoja na madaktari kutoka Hospitali ya Ostrava iliyopo Jamhuri ya Watu wa Czech baada ya kufanya ziara katika taasisi hiyo kuona namna ambavyo wanaweza kushirikiana katika kutoa huduma za matibabu ya moyo jana Jijini Dar es Salaam


XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ipo mbioni kuanzisha ushirikiano katika kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa kushirikiana na madaktari kutoka Hospitali ya Ostrava iliyopo Jamhuri ya Watu wa Czech.

Akizungumza baada ya kufanya ziara JKCI jana Jijini Dar es Salaam Mkuu wa msafara wa madaktari sita kutoka nchini Czech Miroslav Homza amesema kuwa lengo kuu wa madaktari hao kufika JKCI ni pamoja na kuangalia jinsi ambavyo wataweza kushirikiana katika kutoa huduma za matibabu ya moyo ikiwa ni njia ya kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na Czech.

“Tumefika hapa JKCI na kukutana na uongozi kujadilina juu ya uwezekano wa madaktari kutoka JKCI na wale wa Hospitali ya Ostrava iliyopo Jamhuri wa watu wa Czech kuweza kubadilishana uzoefu katika kutoa huduma za matibabu ya moyo haswa upande wa upasuaji wa moyo”,

“Sambamba na kutoa huduma za matibabu ya moyo pia tutaangalia namna gani tunaweza kushirikiana upande wa utafiti katika masuala ya magonjwa ya moyo kati yetu na Tanzania”, alisema Homza.

Aidha Homza amesema kuwa katika ushirikiano huo Czech itaangalia kama kuna uwezekano wa wagonjwa ambao wapo Tanzania na wanahitaji huduma za matibabu ya kina kuchukuliwa na kupelekwa Jamhuri ya watu wa Czech kwa ajili ya matibabu hayo kwani Czech inatoa huduma za matibabu ya hali ya juu na kwa gharama nafuu tofauti na nchi nyingine duniani.

Akizungumzia ushirikianao wa kutoa huduma za matibabu ya moyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi alisema kuwa JKCI imekua ikishirikiana na madaktari kutoka nchi mbalibmali ikiwa ni sehemu ya kuongeza uzoefu na kutoa hudama bora na za kibingwa za matibabu ya moyo.

“Leo tumepokea madaktari kutoka Jamhuri ya watu wa Czech ambao wamefika kujadiliana nasi namna ambavyo tutashirikiana katika kubadilishana uzoefu wa kutoa huduma za matibabu ya moyo, Tumekubaliana kuandaa makataba wa makubaliano ambao utatuongoza katika kushirikiana na kufaidia katika kubadilishana uzoefu huo”, alisema Prof. Janabi 

 

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari