EAC, SADC wakaribishwa JKCI kutibiwa magonjwa ya moyo
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Stella Mongela akiwaonesha viongozi wa wizara zinazosimamia vituo vya umahiri (center of excellence) pamoja na viongozi wa vituo hivyo kutoka nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) jinsi tundu lililoko kwenye moyo linavyozibwa kwa kutumia mtambo wa Cathlab wakati viongozi hao walipotembelea JKCI kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akielezea huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na taasisi hiyo kwa viongozi wa wizara zinazosimamia vituo vya umahiri (center of excellence) pamoja na viongozi wa vituo hivyo kutoka nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) na wataalamu wa afya kutoka Hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia walipotembelea Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya viongozi wa wizara zinazosimamia vituo vya umahiri (center of excellence) p...