Hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia yatembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kuangalia huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Prof. Mohamed Janabi akielezea namna ambavyo JKCI inatoa huduma kwa wagonjwa
wakati wa ziara ya viongozi kutoka Hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia
walipotembelea JKCI kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo
zinazotolewa na taasisi hiyo leo katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya viongozi kutoka Hospitali ya Taifa ya Moyo iliyopo
nchini Zambia wakisikiliza taarifa iliyokuwa inatolewa na Prof. Janabi (hayupo
pichani) wakati wa ziara ya viongozi hao kuangalia huduma za matibabu ya moyo
zinazotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo katika ukumbi wa
Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Makamu wa Chuo Kikuu cha Afya ya Sayansi Muhimbili Prof.
Andrea Pembe akizungumza na uongozi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) ulioambatana na viongozi kutoka Hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini
Zambia kwa ajili ya kuona namna ambavyo watashirikiana katika masuala ya
taaluma baada ya viongozi hao kutembelea JKCI kuangalia huduma za matibabu ya
moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam
Msimamizi wa wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo ambaye pia
ni Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tedy Tarimo akielezea
majukumu ya wodi hiyo kwa viongozi kutoka Hospitali ya Taifa ya Moyo ya Nchini
Zambia walipotembelea wodi hiyo kuangalia huduma za matibabu ya moyo
zinazotolewa leo katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Msimamizi wa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum
(ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Abela Venance akimuonesha namna
ambavyo taarifa za mgonjwa huandikwa Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi kutoka Hospitali
ya Taifa ya Moyo ya Nchini Zambia Josephine Chimpinde wakati wa ziara ya
viongozi kutoka hospitali hiyo walipotembelea JKCI kwa ajili kuangalia huduma
za matibabu ya moyo zinazotolewa na taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka Hospitali
ya Taifa ya Moyo ya Nchini Zambia walipotembelea JKCI kwa ajili ya kuangalia
huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na taasisi hiyo leo Jijini Dar es
Salaam
Picha na: JKCI
Comments
Post a Comment