Raia wa Ujerumani mbioni kutibiwa JKCI
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimuonesha moja ya chumba cha kulaza wagonjwa mashuhuri (VIP Room) Daktari kutoka ubalozi wa Ujerumani kanda ya Afrika Mashariki na Kati Jorg Siedenburg wakati alipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuangalia huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo. Lengo la kufanya ziara hiyo ni kuona namna ambavyo wafanyakazi wa balozi na watalii kutoka Ujerumani wanaotembelea nchi za Afrika Mashariki na kati pale watakapohitaji huduma za matibabu ya moyo watatibiwa JKCI.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Tatizo Waane akimwelezea huduma zinazotolewa kwa wagonjwa wa nje
Daktari kutoka ubalozi wa Ujerumani kanda ya Afrika Mashariki na Kati Jorg
Siedenburg alipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuangalia huduma
zinazotolewa na JKCI. Lengo la kufanya ziara hiyo ni kuona namna ambavyo
wafanyakazi wa balozi na watalii kutoka Ujerumani wanaotembelea nchi za Afrika
Mashariki na kati pale watakapohitaji huduma za matibabu ya moyo watatibiwa
JKCI.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tulizo Shemu akimuonesha jinsi uzibuajia wa mishipa ya damu ya moyo unavyofanyika kwa kutumia mtambo wa Cathlab Daktari kutoka ubalozi wa Ujerumani kanda ya Afrika Mashariki na Kati Jorg Siedenburg wakati alipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuangalia huduma zinazotolewa. Lengo la kufanya ziara hiyo ni kuona namna ambavyo wafanyakazi wa balozi na watalii kutoka Ujerumani wanaotembelea nchi za Afrika Mashariki na kati pale watakapohitaji huduma za matibabu ya moyo watatibiwa JKCI.
Daktari bingwa wa wagonjwa wa dharula na mahututi wa Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Vivian Mlawi akimwelezea huduma wanazozitoa kwa
watoto waliolazwa katika wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) daktari
kutoka ubalozi wa Ujerumani kanda ya Afrika Mashariki na Kati Jorg Siedenburg
wakati alipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuangalia huduma mbalimbali
zinazotolewa. Lengo la kufanya ziara hiyo ni kuona namna ambavyo wafanyakazi wa
balozi na watalii kutoka Ujerumani wanaotembelea nchi za Afrika Mashariki na
kati pale watakapohitaji huduma za matibabu ya moyo watatibiwa JKCI.
***********************************************
Picha na: JKCI
Comments
Post a Comment