Wagonjwa saba wenye tatizo la hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo watibiwa katika kambi maalum ya matibabu ya moyo
Wagonjwa saba wenye tatizo la hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo wamepatiwa matibabu katika kambi maalum ya matibabu iliyofanywa na wataalamu mabingwa wa mfumo wa umeme wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka Hospitali ya Shifa iliyopo nchini Misri.
Akizungumzia
kuhusu kambi hiyo iliyomalizika hivi karibuni daktari bingwa wa mfumo wa umeme
wa moyo kutoka JKCI Yona Gandye alisema kambi hiyo ya siku mbili ilikuwa maalum
kwaajili ya kutoa tiba kwa wagonjwa pamoja na kutoa mafunzo kwa madaktari na wataalamu wengine wa Taasisi hiyo.
Dkt.
Gandye alisema matibabu ya wagonjwa hayo waliyagawa katika makundi matatu
ambapo kundi la kwanza ni la wagonjwa ambao moyo ulishindwa kufanya kazi
ukiambatana na tatizo la hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo unaokwenda taratibu
(Heart failure & slow electrical conduction). Wagonjwa hao walipandikizwa kifaa kinachojulikana kwa jina la Cardiac
Resynchronical Therapy – CRTD) kinachotumia umeme mkubwa (High Power Device).
“Kifaa
hiki cha CRTD ambacho waliwekewa wagonjwa watatu kinasawazisha mgawanyiko wa
umeme wa moyo kufanya kazi kwa pamoja (Synchronization). Uwekaji wa kifaa hiki
unatumia zaidi ya saa moja kutegemeana na tatizo alilokuwa nalo mgonjwa”,
alisema Dkt. Gandye.
Kundi
la pili la wagonjwa waliotibiwa katika kambi hiyo ni wale waliokuwa na tatizo
la hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo
unaosababisha mapigo ya moyo kwenda haraka kuliko kawaida ambapo matibabu yao
yalichukuwa zaidi ya masaa mawili.
Dkt.
Gandye alisema, “Wagonjwa hawa ambao
walikuwa watatu walipata huduma ya matibabu ambayo kwa kitaalamu yanajulikana
kwa jina la EP Study & ablation ambapo wataalamu kwa kutumia vifaa maalum vilivyopo
katika mtambo wa Carto 3 System 3D & Conventional System wanauwezo wa kutambua sehemu ambayo hitilafu ya umeme inapotokea
na kisha kuithibiti ili hali hiyo
isitokee tena”,.
“Kundi
la tatu lilikuwa ni la mgonjwa mmoja kutoka Zanzibar aliyekuwa na tatizo la
umeme wa moyo kwenda taratibu (Atrial Fibrillation with slow Ventricular
response) na kuwekewa kifaa cha kuusaidia moyo kufanya kazi ambacho kwa jina la
kitaalamu kinajulikana kwa jina la Pacemaker”,.
Dkt.
Gandye alisema hali za wagonjwa zinaendelea vizuri na kuna wagonjwa ambao
wamesharuhusiwa na kurudi nyumbani na wengine wataruhusiwa siku chache zijazo.
Kwa
upande wake daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na matibabu ya mfumo wa umeme wa
moyo Prof. Mervat Aboulmaaty kutoka Hospitali ya Shifa iliyopo nchini Misri
aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kufunga vifaa tiba vya kisasa katika
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kusomesha wataalamu ambao wanatoa
huduma za matibabu ya kibigwa kwa wananchi.
Prof.
Mervat alisema kambi hiyo pamoja na kutoa
matibabu kwa wagonjwa pia ilienda sambamba na ubadilishanaji wa ujuzi wa kazi pamoja
na kutoa mafunzo kwa wataalamu wa afya ndani na nje ya nchi.
“Wakati
tunafanya matibabu ya upandikizaji wa kifaa cha CRTD yalirushwa moja kwa moja
kwa njia ya satellite kupitia mtandao wa Zoom kutokea katika mtambo wa Cathlab
(Catheterization Laboratory) ambayo ni maabara ya uchunguzi na tiba ya magonjwa
ya moyo inayotumia mionzi maalum uliopo
hapa JKCI Tanzania ambapo wataalamu 42 waliweza kuona moja kwa moja tulichokuwa
tunakifanya”,.
“Pia
tulitoa mafunzo kwa njia ya mtandao wa
Zoom kuhusu matibabu ya mfumo wa umeme wa moyo na upandikizaji wa kifaa cha
CRTD ambapo wataalamu zaidi ya 291 walihudhuria na kuweza kuuliza maswali
mbalimbali kwa njia ya ujumbe fupi wa maandishi. Kutoa mafunzo kwa njia hii
kunasaidia kwa kiasi kikubwa elimu hii
kuwafikia watu wengi zaidi ndani na nje ya nchi”, alisema Prof. Mervat.
Kwa
upande wake Sabina Machange ambaye ni
mwalimu mstaafu alishukuru kwa huduma alizozipata na kusema kwa muda wa miaka
mitatu amekuwa na tatizo la kutokupumua vizuri, kuvimba tumbo na miguu baada ya kufanyiwa uchunguzi wataalamu walimwambia
moyo wake haufanyi kazi vizuri na hivyo
kutakiwa kuwekewa kifaa cha kuusaidia moyo kufanya kazi vizuri CRTD.
“Jumatano
ya tarehe 23 mwezi huu nilifanyiwa upasuaji mdogo na kuwekewa kifaa hiki, sasa hivi
ninajisikia vizuri nilikuwa siwezi kuinama kabisa lakini sasa hivi ninainama
bila shida, nilikuwa siwezi kupumua vizuri sasa hivi ninapumua bila wasiwasi.
Leo hii nimeruhusiwa, daktari ameniambia
nirudi kliniki jumanne ijayo”,.
Mama
Sabina alisema changamoto kubwa aliyokutana nayo ni gharama kubwa ya matibabu
na kuambiwa kuwa bima ya taifa ya afya (NHIF) ambayo anaitumia hailipii
matibabu hayo na kuiomba Serikali iangalie ni namna gani itawasaidia wagonjwa
wenye matatizo kama yake ili waweze kupata matibabu.
“Niliambiwa
gharama ya kuwekewa kifaa hiki ni shilingi milioni 29 na laki mbili nikaenda makao
makuu ya mfuko wa taifa wa bima ya afya Dodoma na kuwaandikia barua ili
wanilipie nusu gharama wakanijibu kwa barua kuwa utaratibu huo haupo”,.
“Lakini
ndugu na jamaa zangu walinichangia fedha,
nikaweza kulipia nikawekewa kifaa hiki. Ninaiomba Serikali kupitia mfuko wa
Taifa wa bima ya afya ishiriki kulipia hata kwenye matibabu yenye gharama kubwa
kwa kuchangia japo nusu gharama”, alisema Mama Sabina.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed
Janabi alimshukuru Prof. Mervat na timu yake ya madaktari wawili kutoka nchini Misri
kwa huduma waliyotoa kwa wagonjwa na kuweza kuokoa maisha yao.
“Ninawashukuru
madaktari, wauguzi pamoja na mafundi sanifu wa moyo (Technician) wa Cathlab kwa
ushirikiano mzuri waliouonesha kwa wageni wetu pamoja na kupokea mafunzo
yaliyotolewa na wataalamu hao pia kwa
huduma nzuri waliyoitoa kwa wagonjwa ambao walipatiwa matibabu katika
kambi hii”, alishukuru Prof. Janabi.
Comments
Post a Comment