Wagonjwa 20 wafanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo katika kambi maalum ya matibabu iliyofanywa na madaktari wa JKCI na mwenzao kutoka Hospitali ya Max iliyopo nchini India
Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na mwenzao kutoka Hospitali ya Max ya nchini India Dkt. Subhash Sinha wakimbadilisha mshipa mkubwa wa moyo (Aorta) mgonjwa ambaye mshipa wake uliokua umetanuka zaidi ya sentimita 5 wakati wa kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku saba iliyofanyika katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Jumla ya wagonjwa 20 wamefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo Wataalam wa Afya kutoka Idara ya Upasuaji mkubwa wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kutoka hospitali ya Max iliyopo nchini India Subhash Sinha baada ya kumalizika kwa kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku saba iliyofanyika katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Na: JKCI ********************************************************************************************* Wagonjwa 20 wamefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo wa kuf...