Wafanyakazi bora wa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2021/2022 wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wapongezwa kwa utendaji mzuri wa kazi

Mfanyakazi bora wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Afisa Muuguzi Joshua Ogutu akipokea cheti cha mfanyakazi bora kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt. Delilah Kimambo wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora leo katika Ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.

Mfanyakazi bora wa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2021/2022 aliyeshika nafasi ya kwanza Afisa Msaidi wa Afya Dominick Kanani katika picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo na Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji Dkt. Angela Muhozya wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora leo katika Ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam

Mfanyakazi bora wa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2021/2022 aliyeshika nafasi ya pili Mtunza Kumbukumbu (Afya) Vedastus Lazaro akipokea cheti cha mfanyakazi bora kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora leo katika Ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.


Mfanyakazi bora wa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2021/2022 aliyeshika nafasi ya tatu Mhasibu Mohamed Isimbula katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Fedha na Mipango wa JKCI Agnes Kuhenga baada ya kupokea cheti cha mfanyakazi bora wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora leo katika Ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam

Picha na: JKCI
***********************************************************************
 

Comments

Popular posts from this blog

Wateja wa CRDB kutibiwa JKCI kwa punguzo la asilimia 50%

Wanawake wa JKCI SACCOS wanaongoza kwa kumiliki hisa

JKCI kutanua huduma za matibabu ya moyo nchini