Posts

Showing posts from December, 2022

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kuwahudumia watanzania kwa masaa 24

Image

Dkt. Kisenge ahimiza ushirikiano katika kutoa huduma bora

Image
  Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo akitoa taarifa ya kazi zilizofanywa na Taasisi hiyo kwa kipindi cha Januari hadi Novemba 2022 katika kikao cha wafanyakazi wa JKCI kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akijibu swali katika kikao cha wafanyakazi wa Taasisi hiyo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete JKCI wakisikiliza kwa umakini uwasilishwaji wa taarifa ya kazi zilizofanywa na Taasisi hiyo kwa kipindi cha Januari hadi Novemba 2022 katika kikao cha wafanyakazi kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. ***************************************************************************************************************************************************************  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge amehimiza kuimarisha ushirikiano kwa wafanyakazi wa Taas

Wafanya mazoezi ya kutembea Km.7 kulinda afya za mioyo yao

Image
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delila Kimambo akiwaongoza wafanyakazi wa JKCI pamoja na wanachama wa kikundi cha Wasafi Jogging Club kufanya mazoezi ya mbio za taratibu (Jogging) za umbali wa Km. 7 ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza inayofanywa na Taasisi hiyo yenye  kauli mbiu  “Tembea na JKCI,Linda Afya ya Moyo Wako” .  Matembezi hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salam. Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na wanachama wa kikundi cha Wasafi Jogging Club wakifanya mazoezi ya viungo kabla ya kuanza kwa mbio za taratibu (Jogging) za umbali wa Km.7 ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza inayofanywa na Taasisi hiyo yenye  kauli mbiu “Tembea na JKCI,Linda Afya ya Moyo Wako” . Matembezi hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salam. Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na wanachama wa kikundi cha Wasafi Jogging Club wakifanya mazo

Dkt. Kisenge: Jiendelezeni kielimu ili muendane na teknolojia ya matibabu

Image
Mkurugenzi wa   Fedha na Mipango wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA. Agnes Kuhenga akiwasilisha rasimu ya bajeti ya Taasisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24 wakati wa kikao na viongozi wa JKCI cha kupitia na kujadili bajeti ya Taasisi hiyo ya mwaka wa fedha 2023/24 kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akielezea namna ambavyo JKCI itatekeleza  majukumu yake wakati wa kikao cha viongozi wa Taasisi hiyo cha  kupitia na kujadili rasimu ya bajeti ya JKCI kwa  mwaka wa fedha wa 2023/24 kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Kitengo cha Mipango wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Vida Mushi akiwasilisha baadhi ya vifungu vilivyopo katika bajeti ya Taasisi hiyo wakati wa kikao cha viongozi wa Taasisi hiyo cha kupitia na kujadili rasimu ya bajeti ya Taasisi ya mwaka wa fedha 2023/24 kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. Baadhi ya Viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

JKCI kushiriki maonesho ya kimataifa nchini Comoro

Image
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza kuhusu JKCI kushiriki maonesho ya kimataifa nchini Comoro ********************************************************************************************************************************************* Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inatarajia kushiriki maonesho ya bidhaa na huduma zinazozalishwa Tanzania yanatakayofanyika nchini Comoro kuanzia tarehe 10 hadi tarehe 20 Desemba mwaka huu. Katika maonesho hayo Taasisi hiyo itaonesha huduma za kibingwa za matibabu ya moyo inazozitoa kwa wananchi wa Comoro. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt. Peter Kisenge alisema Taasisi hiyo imeona ni muhimu kushiriki katika maonesho hayo ili kutangaza huduma za kibingwa za matibabu ya moyo ambazo zimekuwa zikihitajika na watu kutoka nchini humo.   Dkt. Kisenge alisema JKCI imeendelea kukuwa kwa kasi na kuwa bora Afrika Mashariki na kati hivy

Naibu Katibu Mkuu Afya atembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

Image
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya leo katika Taasisi hiyo iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt. Peter Kisenge. Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tulizo Shemu akielezea namna ambavyo wagonjwa wa nje wanavyohudumiwa wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akielezea namna  huduma za matibabu zinavyotolewa kwa wogonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Ghati Chacha akitoa  

JKCI kutoa matibabu bure kwa watakaofanya vizuri katika kampeni ya “Tembea na JKCI, Linda Afya ya Moyo Wako”

Image
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu akizindua kampeni ya kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete yenye kaulimbiu “Tembea na JKCI, Linda Afya ya Moyo Wako”. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu kitabu cha mtindo bora wa Maisha wakati wa uzinduzi wa  kampeni ya kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza uliofanyika hivi karibuni katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete yenye kaulimbiu  “Tembea na JKCI, Linda Afya ya Moyo Wako”. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wananchi waliofika katika viwanja vya Taasisi hiyo kwa ajili ya kufanya mazoezi ya  kutembea umbali wa Km. 5 wakati wa uzinduzi wa  kampeni ya kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza uliofanyika hivi karibuni katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwet

Ngusa: Tumieni vizuri ujio wa madaktari bingwa wa moyo kuchunguza afya zenu

Image
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Ally Athuman akimpima shinikizo la damu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Ngusa Samike alipofika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi Sokoine (SRRH) kwa ajili ya kufungua kambi maalum ya siku tatu ya matibabu ya moyo inayofanywa na wataalam wa afya wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa SRRH Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Nuru Letara akimwelezea Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Ngusa Samike huduma zinazotolewa kwa watoto wenye magonjwa ya moyo alipofika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi Sokoine (SRRH) kwa ajili ya kufungua kambi maalum ya siku tatu ya matibabu ya moyo inayofanywa na wataalam wa afya wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa SRRH. Wanne kutoka kushoto ni Mganga Mfawidhi wa SRRH Dkt. Mohamed Muhaji Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Khairoon Mohamed akimfanyia uchunguzi mama ambaye amepata kiharusi wakati wa kambi maalum ya siku tatu ya uchunguzi na

Watu 429 wafanyiwa uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo Mkoani Mtwara

Image
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Ally Athuman akimpima wingi wa sukari mwilini mwananchi wa Mkoa wa Mtwara aliyefika katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini (SZRH) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tatu iliyokua ikifanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa SZRH na kumalizika jana kwa kuwafanyia uchunguzi na matibabu ya moyo wananchi 429. Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Janeth Mmari akiwaelezea namna ya kujikinga na magonjwa ya moyo wananchi wa Mkoa wa Mtwara waliofika katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini (SZRH) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tatu iliyomalizika jana kwa kuwafanyia uchunguzi na matibabu ya moyo wananchi 429. Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Nuru Letara akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) mtoto aliyefika katika